Laptop ya kwanza Duniani? Imepewa sifa hiyo, Ifahamu Toshiba T1100

Toshiba T1100 – Ifahamu Laptop ya Kwanza Kuweza Nunuliwa na Mtu Yeyote Duniani

0
Sambaza

Ijue Toshiba T1100. Ni takribani miaka 31 sasa na laptop ya kwanza duniani kuweza kuuzika kwa watumiaji wowote (mass market) na leo fahamu sifa zake.

Kabla ya mwaka 1985 tayari matoleo kadhaa ya laptop chache na zilizouzwa kwa mashirika machache kama vile jeshi n.k tayari yalishatoka lakini ni ujio wa laptop ya Toshiba T1100 ndio ukastahili sifa kamili ya kuwa laptop ya kwanza kabisa kuanza kupatikana sokoni.

Toshiba T1100 Laptop ya kwanza duniani

Muonekano wa laptop ya Toshiba T1100

Laptop hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Toshiba ya nchini Japan ilijipatia umaarufu na inachukuliwa kama moja ya laptop zilizoleta mabadiliko sana katika teknolojia na uanzashwaji wa utengenezaji wa laptop kwa ajili ya watumiaji wa aina zote.

INAYOHUSIANA  Microsoft na WhatsApp waunganisha nguvu kufanya kitu

Sifa zake za ndani kwa kipindi hicho zilikuwa zinazotosha tuu kwa watumiaji mbalimbali ingawa buy doxycycline online uk kwa sasa simu janja yako tuu itakuwa inauwezo mara maelfu kuizidi laptop hii.

Ilikuja na;

  • RAM ya click KB 256
  • Prosesa – 4.77 MHz Intel Processor
  • Haikuwa na ‘HDD’ – Hard disk, ilikuwa inatumia Floppy Disk
  • Programu endeshaji ya MS DOS
  • Ilikuwa na here uzito wa kg 4.1
Toshiba T1100

Toshiba T1100, Muonekano wa eneo la kuweka Floppy Disk. Toleo spesheli la Toshiba T1100PLUS lilikuwa na maongezo kama vile maeneo mawili ya Floppy disk na RAM ya KB 640. Kwa matumizi makubwa.

Ndani ya mwaka wake wa kwanza kupatikana Toshiba waliuza laptop hizo 10,000, nyingi zikienda barani Ulaya…na zikajipatia sifa ya kipekee kama laptop ya kwanza kuweza kutumika na watu kwa matumizi mbalimbali madogo na makubwa ukilinganisha na kabla ya hapo.

INAYOHUSIANA  Downloading vs Streaming : Fahamu Tofauti Kuu, Kipi bora zaidi?

Kwa kipindi hicho mtu kumiliki laptop hiyo ilikuwa ni bonge la maendeleo, unaweza fananisha na mtu kumiliki laptop za kisasa kabisa za siku hizi kama vile MacBook Air, Surface n.k

Laptop hiyo ilikuwa ikiuzika wa takribani dola 1899 za kimarekani – Tsh 4,158,000 | Ksh 192,359…. kwa bei hiyo kwa sasa unapata laptop ya kiwango kikubwa sana.

Je ulikuwa unafahamu kuhusu laptop hii? Tuambie maoni yako kupitia eneo la comment

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.