Toyota ni kampuni kubwa sana ya magari duniani ambayo asili yake ni Japan. Toyota ni kampuni ambayo ina aina nyingi za magari na imekua ni kimbilio la wengi kwa nchi masikini.
Licha ya kuwa na magari ya kifahari na yale ya kawaida bado kampuni haijapumzika, bado inajituma kuhakikisha kuwa inawapatia wateja wake kile ambacho wanastahili.
Kwa sasa kampuni imekuja na mpya na kusema kuwa wako katika mchakato endelevu wa kutengeneza magari ambayo yataweza kupaa. Vilevile wanafanya hivi ili magari hayo yatumike katika mashindano ya olimpiki mwaka 2020.
Ukiachana na mashindano hayo kama kampuni itafanikisha zoezi hili na magari yakitengenezwa na yakapita vipimo vyote vya endeshaji basi magari hayo yataweza kuingia sokoni mwaka 2023.
Hii ni baada ya kujaribiwa mwaka 2019 na kutumika kidogo katika mashindano ya olimpiki mwaka 2020 na kuzalishwa kwa wingi na kuuzwa mwaka huo (2023).
“Nimekua nikipenda magari na ndege. Na kwa kipindi cha muda mrefu nimekua nikipenda kuwa na usafiri ambao unaweza kupaa kutoka sehemu moja hadi nyingi” — Alisema mkuu wa projekti hiyo, Tsubasa Nakamura
Kama hujui unaweza ukasema Toyota wameanza jambo hili hivi karibuni lakini ukweli ni kwamba zoezi hili lilianza tangia mwaka 2012.
Angalia Hii
Mpaka sasa Nakamura na timu yake wameweza kurusha mfano wa gari hadi usawa wa macho tuu na matumaini yao ni kwamba wataweza kulirusha juu zaidi ya hapo.