Kwanini TTCL yakanusha kuhusika na matatizo ya tiketi za mwendokasi

TTCL yakanusha kuhusika na matatizo ya tiketi za mwendokasi

0
Sambaza

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limekanusha kuhusika na matatizo ya huduma za tiketi kwa mabasi ya mwendokasi (UDART) jijini Dar Es Salaam.

source url

Kwa muda wa wiki sasa kumekuwa na matatizo katika ukatishaji tiketi wa mabasi ya mwendokasi ambapo imekuwa kero na usumbufu kwa wananchi wanaotumia huduma za mabasi ya mwendokasi.

TTCL kupitia taarifa iliyoitoa wiki hii imesema kwamba shirika hilo source link halihusiki na chochote zaidi ya kutoa huduma za mfumo wa mawasiliano kielektroniki (Internet Connectivity na Network Support) ambayo inatolewa kwa ufanisi mkubwa.

Taarifa hiyo imesema TTCL sio wahusika katika uuzaji na usimamiaji wa huduma za tiketi kwenye mabasi ya yanayotumia njia za mwendokasi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Aidha, TTCL imeongeza kusema haiwezi kuingia mkataba na UDART bila ya maridhiano na DART kama sheria na kanuni zinavyoelekeza.

matatizo ya tiketi za mwendokasi

TTicketi ya muda kwa mabasi ya mwendokasi inayotumika hivi sasa baada ya follow link Maxcom kumaliza mkataba wake na UDART.

Mwisho, taarifa hiyo imesema TTCL ni shirika la serikali kwahiyo mara zote itasimamia maslahi ya umma na wakati wote itaendelea kuweka mbele utoaji wa huduma bora kwa taifa.

INAYOHUSIANA  Bakhresa aanzisha kampuni ya mawasiliano ya simu-Azam Telecom

Ni vyema wahusika wakaweka mambo sawa ili huduma hiyo iweze kurejea katika ufanisi wake. Ni wazi kuwa huduma ya mabasi yaendayo haraka (BRT) imerahisisha watu kuweza kufika maeneo mbalimbali jijini Dar ndani ya muda mchache.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.