TTCL kujenga kiwanda cha utengenezaji simu nchini - TeknoKona Teknolojia Tanzania

TTCL kujenga kiwanda cha utengenezaji simu nchini

0
Sambaza

Kampuni ya simu ya TTCL imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha uzalisha wa simu za kisasa nchini Tanzania.

source site

follow link Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya simu ya TTCL Waziri Waziri Kindamba alisema kwa sasa wanazungumza na washirika watakao kuwa nao katika kufanikisha azma hiyo; lengo hilo ni kusaidia mwelekeo wa nchi kuwa ya viwanda na uchumi wa kati. Hata hivyo hakutaja ni washirika gani watakafanikisha mpango huo.

Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya simu ya TTCL Waziri Waziri Kindamba

Kuwepo kwa kiwanda cha simu nchini itasaidia kwa kila mwanachi kuweza kumiliki simu kwa kuwa zitauzwa kwa bei ya kiwango cha chini tofauti na simu zinazozwa kutoka nchi Amerika, Asia na Ulaya.

Prozac Mafanikio ya ujenzi wa kiwanda hicho cha simu  nchini Tanzania itamfanya mwananchi ajihisi fahari ya kutumia simu inayozalishwa na kampuni ya kizalendo. Kwa sasa Kampuni ya TTCL inamilikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 baada ya kununua hisa zote za kampuni ya Bharti Airtel iliyokuwa mbia mwenza wa TTCL.

TTCL inaonekana kudhamiria kurudisha heshima yake iliyokuwanayo huko nyuma na kwa mipango ya kujenga kiwanda chake mwenywe itakuwa ni jambo la kujivunia na kuwa chachu ya maendeleo ya nchi nzima na uchumi kwa ujumla.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Apple kufanyia matengenezo bidhaa zao bure
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.