Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka itaanza kutumia mfumo wa malipo ya nauli kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL badala ya Kampuni ya Maxcom Afrika ambayo ilikuwa inafanya shughuli hiyo tangu awali.
Kupitia Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa UDART, Deus Bugaywa amesema hatua ya kutumia TTCL ni baada ya mkataba wao na Maxcom Afrika kuisha na hivyo kuwatumia TTCL kutokana na kuboreshwa kwa huduma zake na pia ni Shirika lilio chini ya Serikali.
Wanaamini kupitia TTCL ambao huduma zao kuwa katika mkongo wa taifa wateja wao watapata huduma iliyo bora zaidi ya awali.
Kuhusu wafanyakazi waliokuwa wakikatisha tiketi wataendelea na ajira zao na mshahara watapewa na UDART ila watakuwa wanaripoti TTCL badala ya Maxcom.