TTCL waachana rasmi na teknolojia ya CDMA, sasa ni 3G na 4G tuu

TTCL waachana rasmi na teknolojia ya CDMA, sasa ni 3G na 4G tuu

0
Sambaza

Mtandao wa simu wa TTCL umekuwa kwa muda mrefu tuu ukitegemea mfumo wa mawasiliano wa CDMA na sasa mwisho wake umefika.

TTCL waachana rasmi na teknolojia ya CDMA na kuanza kutumia mifumo ya 3G na 4G pekee.

http://thethriveblog.net/ Uamuzi huu ni mzuri kwani kwa kipindi kirefu ilikuwa imefanya kuwa vigumu watumiaji wa mitandao mengine kununua laini ya TTCL na kuweka kwenye simu zao na kuhama mtandao moja kwa moja. Kutumia laini za simu za TTCL ilikuwa inakubidi ununue simu spesheli inayokuja na teknolojia ya CDMA pia.

TTCL waachana rasmi na teknolojia ya CDMA

http://airaligned.org/new-fall-2016-weekly-classes/ TTCL waachana rasmi na teknolojia ya CDMA: Taarifa rasmi kutoka TTCL

click here Teknolojia ya CDMA kwa muda mrefu ilikuwa ni kikwazo kwa TTCL kuweza kuwavutia kwa urahisi watumiaji wapya – waweze kuhamia mtandao huo bila gharama zaidi.

INAYOHUSIANA  TTCL yawapa serikali gawio la Tsh 1.5 bilioni

Pia teknolojia ya CDMA ipo nyuma kidogo kwenye teknolojia za intaneti ya kasi zaidi ukilinganisha na mfumo wa teknolojia wa 3G na ule wa 4G.

Mitambo ya CDMA imezimwa rasmi leo na kwa kiasi kikubwa wateja wa TTCL wa muda mrefu wanaotumia vifaa vya CDMA suala hili litamaanisha wana kipindi kigumu kifedha kwani itawabidi wanunua vifaa vipya ili kuweza kuendelea kutumia huduma za TTCL.

Vipi je wewe una mtazamo gani juu ya uamuzi huu?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.