TTCL Yaanza Kutangaza Kwa Kasi Huduma yao ya 4G Jijini Dar es Salaam

1

Sambaza

Mwaka 2016 umeanza na inaonekana katika mitandao itakayokuwa na kazi kubwa a.k.a u’busy sana kwa mwaka huu ni pamoja na TTCL.

Hivi karibuni tayari serikali ilishasema ubia kati ya TTCL na wamiliki wa Airtel unafikia mwisho rasmi. Hii ni habari nzuri kwa wapenzi wengi mtandao wa TTCL kwani wengi waliamini ubia huo ulikuwa unaigharimu TTCL na si kuusaidia mtandao huo kukua.

Kwa miaka kadhaa mtandao wa TTCL umekuwa kama umelala lakini mwaka huu utakuwa ‘busy’ ukijitoa katika miaka mingi ya kutojitangaza katika soko lililo na ushindani mkubwa na pia kuja kisasa zaidi kwani wana kuja na teknolojia za kisasa zaidi.

INAYOHUSIANA  Ijue sheria ya makosa ya mtandao mwaka 2015

4G LTE jijini Dar es Salaam!

Kama upo jijini Dar es Salaam na unazunguka zunguka basi utakuwa tayari ushakutana na mabango haya

Kama upo jijini Dar es Salaam na unazunguka zunguka basi utakuwa tayari ushakutana na mabango haya

Tayari hivi karibuni walishatangaza rasmi kuanza kutoa huduma ya intaneti ya kasi ya 4G katika baadhi ya maeneo hasa hasa ya mjini Jijini Dar es Salaam. Na pia kupitia mkataba na benki ya TIB wameshafanikiwa kupata pesa za kusambaza teknolojia ya 3G na 4G katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nchini kote.

Je uamuzi wa kutumia teknolojia za 3G na 4G zitasaidia ukuaji wa shirika hili kongwe?

Ushindani katika soko umekuwa mkubwa sana, katika eneo la 3G mitandao kama Airtel, Tigo, Vodacom na sasa Halotel ni mitandao inayoshindina kwa kasi na tayari wengi wao ni nguli katika eneo la kujitangaza kibiashara – ‘marketing’, eneo ambalo kwa muda mrefu TTCL wamekuwa nyuma. Kwenye 4G kuna Smile na Smart.

INAYOHUSIANA  Muhstakabali wa kuona BURE chaneli za ndani

Kufanikiwa kwa TTCL kutategemea zaidi ni kwa jinsi gani watakubali kubadilika katika uendeshaji na kujitangaza. Uwezo wa kutoa huduma ya uhakika wanayo ila hilo pekee halitoshi katika soko lililojaa ushindani mkubwa sana. Ila kwa sasa wameanza vizuri, muda utatuonesha zaidi!

Je wewe una mtazamo gani? Tungependa kusikia kutoka kwako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Mabadiliko ya kiteknolojia - Wafanyakazi 400 Kupoteza Ajira TTCL

Leave A Reply