Toleo lililotolewa la kwa ajili ya majaribio la WhatsApp katika vifaa vya Android linahusisha kipengele cha Voice Mail
Voice Mail ni uwezo wa mtu wa kuacha ujumbe wa sauti wakati akiwa anakupigia simu. Simu yako inaweza ikawa haipatikani au ikawa haipokelewi basi mtu akawa ana uwezo wa kuweza kukuachia ujumbe flani hivi wa sauti
Kutokana na kwamba WhatsApp wamehusisha kipengele hicho katika toleo lao la majaribu basi sio siri tena kuwa kipengele hicho kipo njiani kupatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp
Kwa wale ambao wapo katika programu spesheli ya watumiaji wa kujaribu baadhi ya App za Android (Android Beta Testing Program) ndio wamekuwa watu wa kwanza kabisa katika kukijaribu kipengele hiki
Toleo namba 2.16.189 la App hiyo ndio limeongezewa hiki kipengele. Mtu unaweza ukasema kuwa ‘aaaah Voice mail kwanza zimepitwa na wakati’ lakini kumbuka huduma hii inaweza ikawa ni ya muhimu sana kwa mfano kama unaongea na wafanya kazi wenzio nje ya nchi
Baada ya simu kukatwa (bila kuongea) au kutopokelewa kabisa kuna machaguo yatatokea katika simu janja yako. Machaguo yatakuwa ni Cancel out of the menu, call back , record voice message sasa hiyo ‘record voice messege’ ni sawa kabisa na kuacha ‘voice mail’
Tukae mkao wa kula kwa ajili ya kusubiria kipengele hiki katika simu zetu. Lakini hapa cha muhimu kutilia maanani ni kwamba kwa kuwa bado huduma hii inafanyiwa majaribu hivyo haimaanishi kuwa itakuja latika vifaa vyetu dhahiri. Yaani tusiwe na asilimia mia moja kwani kitu kinachofanyiwa majaribio kinaweza kisifaulu pia