Wanasayansi waja na tumbo la uzazi la bandia, kuwalea watoto njiti

0
Sambaza

Sayansi ya uzazi inazidi kuwa na mapya kila leo jambo linalopelekea kuleta matumaini katika utatuzi wa changamoto mbalimbali ambazo sekta ya afya na sayansi ya uzazi inakumbananazo.

Kuna wale watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao (kabla ya miezi tisa) jambo ambalo linasababisha wazaliwe huku baadhi ya viungo vyao vikiwa bado havijakamilika ipasavyo na hivyo kuwekwa kwenye chombo maalum (incubator) ambacho joto lake ni sawa na joto la kwenye tumbo la uzazi.

SOMA PIA:  Fikiria Simu Bila Ya Betri, Teknolojia Hii Ipo Katika Hatua Zake Za Kwanza!

Wanasayansi nchini Marekani wamebuni tumbo bandia la kutengeneza ambalo katika siku zijazo linaweza kutumiwa kuwekea watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao, maarufu kama njiti.

tumbo la uzazi bandia

Wanasayansi wamefanikiwa kumkuza mtoto wa kondoo (aliyezaliwa kabla ya muda wake) katika tumbo la uzazi bandia bila matatizo yoyote. Na sasa wapo njiani kutaka teknolojia hiyo itumike kwa vichanga vya binadamu.

Watafiti katika hospitali ya watoto ya Philadephia wanasema lengo lao ni kuweka mazingira ambayo watoto wanaozaliwa kabla muda wao kutimia wanaweza kukuza viungo vyao vya mwilini kama vile mapafu na viungo vyengine.

tumbo la uzazi bandia

Inategemewa teknolojia hii ya tumbo la uzazi bandia itaweza kuokoa afya na uhai wa watoto wengi wanaozaliwa kabla ya muda wao. Mazingira yote yatakuwa karibia sawa na yale ya tumbo la uzazi la mzazi

Kutokana na kwamba watoto wanazaliwa wakiwa njiti na uangalizi wao ni wa hali ya juu sana sitakuwa nimekosea nikisema kuwa sayansi ya kuhifadhi watoto kwenye tumbo la bandia itasaidia sana na hata kuokoa vifo vya watoto. Kifaa hicho kimetengezwa kwa kutumia mfuko wa plastiki, uliojazwa maji ya kutengeza yanayoigiza mazingira ya tumbo la uzazi.

SOMA PIA:  Uzalishwaji wa maji yaliyopo hewani! #Sayansi #Teknolojia

Wanasayansi wanaamini mfuko huo unaweza kuwa tayari kwa majaribio ya binadamu baada ya miaka mitatu mpaka mitano kuanzia sasa.

Vyanzo: BBC, The Verge

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com