Tumia Njia Hizi Kusafisha (Kufuta) Vitu Katika Kompyuta Yako!

1
Sambaza

Kwenye kompyuta uchafu wa kidigitali unaweza ukaifanya isiwe inafanya kazi ipasavyo saa nyingine hata kuipelekea kuwa ‘slow’. Kuna njia madhubuti ambazo zinaweza zikakusaidia kusafisha kompyuta yako (kidigitali) na kuifanya ipige kazi kwa ufanisi zaidi

Siri kubwa ya usafi ni kwamba inavifanya vifaa kuwa na maisha marefu, kama ilivyo kwenye gari, nyumba n.k hata katika kompyuta ni hivyo hivyo tuu.

Unaweza Kufanya Hivyo Kwa Kutumia Programu Zifuatazo:

Should I Remove It? – Kama ukiwa umepakua (install) programu nyingi sana katika kompyuta yako kwa kipindi cha muda mrefu. Utakua bado unaendelea kutumia baadhi ya programu hizo huku zingine zikiwa zinajaza nafasi tuu.

Should I Remove It?

Should I Remove It? Ni programu ambayo inaweza kukusaidia kujua nini ni nini. Hii inamaanisha kuwa ita ‘scan’ program za kompyuta yako yote na kukuambia ni programu zipi ambazo watu katika mtandao walifikiria kuzifuta kwenye vifaa vyao. Ni njia nzuri ya kuweza kugundua kuwa ubakize programu au la

SOMA PIA:  Mambo 8 ambayo si rahisi kujua kwenye simu za Samsung Galaxy

PC Decrapifier – Kompyuta nyingi sana huwa zinakuja zikiwa zimepakiliwa na programu za majaribio (trial) au ‘software’ za bei rahisi. Kwa lugha ya kitaalamu inajulikana kama Bloatware na mara nyingi inaweza ikapunguza nguvu kazi ya kompyuta yako

PC Decrapifier

Uzuri ni kwamba unaweza ukazifutilia mbali kwa kutumia PC Decrapifier. Programu hii inagundua na kufuta yote hayo automatiki. Cha muhimu hapa ni kupitia kila kitu kabla ya kufuta maana saa zingine unaweza ukafuta vile vya umuhimu

SOMA PIA:  Hatua 5 za kubalisha akaunti ya Facebook kuwa ya kibiashara

Revo Uninstaller – Inavyosemekana wakati unasitisha programu (Uninstall) katika kompyuta yako, bado kunakuwa na chembe chembe za data za programu hizo zinabakia katika kompyuta yako. Taarifa hizi zinapokuwa nyingi zinairudisha kompyuta nyuma kiufanisi.

Revo Unistaller

Revo Uninstaller

Kama ukitaka kufuta kitu moja kwa moja bila hata ya kuacha alama basi Revo Uninstaller ndio chaguo sahihi. Inatoa mabaki yote ya programu ambazo hazihitajiki katika kompyuta yako.

Duplicate Cleaner – Hivi ukiwa unazurura katika kompyuta yako ishawahi kukutokea unaona mafaili mawili (muziki, video, sinema, picha n.k) ambayo yanafanana kila kitu. Yaani kuanzia jina mpaka ujazo? Mimi nishawahi. Kwa namna moja au nyingine kuwa na kitu kimoja zaidi ya mara moja kinaweza kujaza nafasi ya uhifadhi. Tumia programu hii kufuta hayo. Cha kufanya ni ku scan na kufuta mafaili ambayo yanajirudia kwa kutumia Duplicate Cleaner. Unaweza ukashangazwa na ujazo ambao utauokoa baada ya zoezi hili.

Duplicate Cleaner

Duplicate Cleaner

Baada ya kukujuza hayo, ni jambo jema kufanya usafi. Ukiwa unafanya usafi wa chumba chako, kumbuka na usafi wa kompyuta yako (usafi wa kidigitali) ili kujua jinsi ya kufanya ule usafi wa nje kama kwenye kioo bofya hapa ili kufahamu namna

SOMA PIA:  Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja

Niandikie sehemu ya comment hapo chini hii umeipokea vipi. Usijifanye hujua kama TeknoKona ndio chanzo chako kikubwa cha habari na masuala mbalimbali yanayohusu teknolojia, tembelea kila siku basi. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com