Tumia Simu Yako Kama Vifaa 10 Tofauti Vya Ki-elektroniki! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tumia Simu Yako Kama Vifaa 10 Tofauti Vya Ki-elektroniki!

0
Sambaza

smartphone-and-tablet

Unaitumia vipi simu-janja yako, kupiga na kupokea simu tuu?. Inasemekana asilimia 80 ya watumiaji wa simu-janja hawatumii simu zao katika asilimia 100 kama inavyotakiwa. wengi huwa wanadownload vitu mbali mbali kama magemu na mitandao ya kijamii na kuingia katika intaneti tuu na wanakua wameridhika. vipi kama kuna vitu vingi unavyoweza tumia ukiwa na simu yako? Basi unakosa vitu vingi sana unavyoweza tumia ukiwa na simu-janja yako.

Sasa fahamu ya kwamba unaweza tumia simu yako kama vifaa vifuatavyo,

buy diflucan pill 1. Tumia Simu-janja Yako Kama Redio Za Mawasiliano (Redio Kolu)

Aplikesheni kama zello (Android, iPhone/iPad,Windows) na  HeyTell (iPhone, Android, Windows) zinasaidi kukuwezesha kutumia simu-janja yako kama redio kolu. zinakuwezesha kutuma meseji za sauti za kugusa na kuongea (push-to-talk) kama redio kolu za ukweli

buy estrace cream 2. Tumia Simu-Janja Yako Kama Kama Remoti Ya Kimataifa

Uamini au usiamini aplikesheni kama IR Remote (Android) na  Dijit (iPhone) zinaweza kukuwezesha kutumia simu-janja yako kama remoti katika vifaa mbalimbali vya ki elektroniki. Kujua zaidi kuhusu kutumia simu yako kama remoti soma hapa

INAYOHUSIANA  Huawei ya pili kimauzo kwa mara ya kwanza

enter 3. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wireless Mouse/Keyboard/Touchpad

Je ushawahi kuwaza kununua ‘wireless keyboard’ au ‘mouse’ lakini ukawa huna hela ya kutosha?. sasa mtandao kama Remotemouse.net unaweza ukakusaidia na ukashusha aplikesheni hiyo kwenye simu yako ya Android au iPhone na pia udownload Aplikesheni nyingine kwa kompyuta yako ili kutumia.

4. Tumia Simu-janja Yako Kama WebCam

Ushawahi kukaa na kufikiria kitu kama hiki (ha!). Unaweza usijue lakini ndio hivyo unaweza fanya simu yako ikawa WebCam ya kompyuta yako. Kuna Aplikesheni nyingi za bure kama WO webcam Lite  (Android) na EpocCam (iphone) zinaweza kukusaidia kutumia simu kama webcam.

5. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wi-Fi Router

Hili linaweza lisikushangaze, simu nyingi za Android na iphone sasa zinakuja na Wi-Fi router ambazo zinaweza msaidia mtumiaji wa simu hiyo kurusha mtandao wa intaneti kwenye simu au kompyuta nyingine. ili kuwasha na kutumia mbinu hii nenda kwenye  Wi-Fi Hotspot settings katika simu yako ya Android au iPhone

INAYOHUSIANA  Kupokea simu ya mwanaume mwingine kwasababisha mke kuuawa na mumewe

6. Tumia Simu-janja Yako Kama GPS

Simu nyingi siku hizi zinakuja na GPS kabisa, lakini aplikesheni kama GPS Status & Toolbox (Android) and Waze (iphone) zinaweza kukusaidia kutumia simu yako kama GPS kabisa.Aplikesheni hizo ni za bure katika Appstore na Google Playstore

7. Tumia Simu-janja Yako Kama Scanner

Mara ngapi umetaka ku scan nyaraka zako na ikakulazimu uende kwenye steshenali kwa  sababu huna scanner? Kwa kutumia Aplikeshi ya simu yako kama CamScanner (Android, iPhone/iPad, Windows 8) huhitaji kuwa na mawazo kwamba utascan wap nyaraka zako. kitu kingine kuhusu aplikesheni hii ni kwamba ni ya bure na unaweza kuscan na nyaraka zako zikawa katika ubora wa hali ya juu

8. Tumia Simu-janja Yako Kama TV

KWa kutumia Aplikesheni kama LiveNow! TV (Android) and PBS (iPhone) unaweza kutumia simu yako kuangalia TV. Aplikesheni zote hizi ni bure katika  masoko ya Android na Apple lakini unatumia Internet Kuangalia TV hiyo katika simu.

INAYOHUSIANA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

9. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wireless PC Speaker

Shusha Aplikesheni kama SoundWire (Android) or Airfoil Speakers Touch (iPhone, iPod, iPad) katika simu yako na kisha shusha software ya aplikeshi hizo katika komyuta yako. KWa kufanya hivyo hapo utaweza kucheza miziki katika simu yako kwa kutumia kompyuta

10. Tumia Simu-Janja Yako Kama Motion detector

Kama simu yako ina sensa, basi unaweza ukafanya mambo mengi ya kuvutia kama kubadili wombo katika simu yako kwa kupitisha mkono juu ya skrini bila kugusa simu. kama una uhakika simu yako ina sensa basi shusha Proximity Actions (Android) au  Smart Player Free (iPhone) kutumia simu yako bili kugusa skrini.

Sasa nina imani unaweza kutumia Simu-janja zako kiujanja zaidi. Kama una wazo lolote ningependa kulisikia kuhusiana na hii makala, tuwasiliano kupitia akaunti zetu za Twitter au Facebook

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply