Turing Phone Cadenza: Simu ina GB 12 za RAM, Kamera MP 60, Uhifadhi TB 1 na laini 4

0
Sambaza

RAM GB 12, Uhifadhi wa GB 1,000…Ni vigumu kuamini simu kuwa na uwezo (specifications) wa kiwango hichi ila simu ya Turing Phone Cadenza iliyopo njiani inavyo.

simu ya turing

Muonekano wa toleo lililopita la simu ya Turing

Simu janja ya Turing Phone Cadenza imetengenezwa na kampuni inayofahamika kwa jina la Turning Robotics Industries ya nchini Marekani.

Sifa kuu- vigumu kudukuliwa, vigumu kuvunjika…hivyo kiwango cha usalama wa juu

Simu za Turing zinatengenezwa pia kwa kutumia madini magumu ya ‘liquidmorphium’ ambayo yanafanya ‘housing’ ya simu hiyo kuwa ngumu sana. Kuvunjika kwa simu hii kutaitaji nguvu ya ziada, madini haya ya chuma ni magumu sana – zaidi ya mara 1.5 ukilinganisha ugumu wa madini ya titanium.

turing phone cadenza

Bei ya simu hii inategemewa kuwa kwenye kati ya Tsh 1,500,000/= – Tsh 2,500,000/=.

Sifa za undani;

  • Inakuja na ukubwa wa inchi 5.8, kioo (display – QHD) .
  • Kamera ina Megapixel 60, na megapixel 20 kwa kamera ya selfi.
  • Itakuja na prosesa mbili za kisasa ndani yake za Snapdragon 830, (prosesa zinategemewa kuanza kupatikana mapema mwakani)
  • Diski uhifadhi (storage) kiasi cha TB 1, ndani kabisa ina GB 512 alafu inakuja na sehemu mbili za memori kadi ya GB 256 kila moja.
  • Ina kiwango cha RAM cha GB 12 – ikiwa na RAM mbili za GB sita sita..hiki ni kiwango cha juu sana, suala la uzito wa vitu kufanya kazi halitawezekana.
  • Unalaini nyingi za simu? Simu hii inauwezo wa kutumia laini 4 ndogo (Nano) kwa wakati mmoja.
  • Programu endeshaji: Inatumia programu endeshaji ya Swordfish OS (toleo la Sailfish OS) lilotengenezwa na kampuni ya Jolla – programu endeshaji hii ilianzaga kwa jina la MeeGo zamani na ilikuwa ‘project’ chini ya kampuni ya Nokia. Programu endeshaji hii imepewa uwezo wa kutumia apps za Android.

simu ya Turing Turing Phone Cadenza

Turing Phone Cadenza imepewa uwezo mkubwa wa kiusalama wa data. Na utumiaji wake wa programu endeshaji ya Swordfish inazidi kuiweka sehemu salama zaidi kiusalama.

Kampuni ya Turin bado haijatoa bei rasmi ya simu janja hiyo ila wamesema itaingia sokoni rasmi mwaka 2017 na tunauhakika bei yake itakuwa juu sana.

Tuambie mtazamo wako juu ya simu janja hii… 

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Apple kuruhusu rasmi makampuni mengine kurekebisha simu zao
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com