Twitter: Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi (DM) kutoka kwa watu wote - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Twitter: Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi (DM) kutoka kwa watu wote

0
Sambaza

Makala hii itakusaidia kufahamu jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji za Inbox (DM) kutoka kwa mtumiaji mwingine yeyote kwenye mtandao wa Twitter, awe anakufollow au hakufollow.

Twitter Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi (DM) kutoka kwa watu wote

Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi (DM) Twitter kutoka kwa watu wote

Kwa sasa hivi kupitia app ya Twitter kuna uwezo wa kutuma ujumbe kupitia Inbox bila sheria ya herufi 140, hivyo unaweza andika ujumbe mrefu kuliko ukitumia njia ya kutweet.

Kwa kawaida ukijiunga tuu Twitter mtandao huu huwa umezuia wewe kupokea ujumbe wa DM kutoka kwa mtumiaji mwingine yeyote – inatakiwa anakufollow na wewe uwe unamfollow.

Tuanze kwa watumiaji mtandao: Twitter.com

INAYOHUSIANA  Programu tumishi kutoka kwa msanii wa Tanzania

Kwa watumiaji wa app ya Android

  • Fungua app, nenda kwenye Settings
  • Kwenye orodha nenda na bofya Privacy and content
  • Angalia na tafuta ‘Receive Direct Messages from Anyone – yaani pokea ujumbe wa moja kwa moja (inbox) kutoka kwa mtu yeyote
  • Bofya kuweka kaalama kuruhusu kupokea ujumbe wa DM kutoka mtu yeyote, ondoa chaguo/alama kuzuia.

Kwenye watumiaji wa app ya iOS

  • Ingia kwenye app na bofya eneo la Me, kisha nenda kwenye Settings
  • Kwenye orodha nenda na bofya Privacy and content
  • Angalia na tafuta ‘Receive Direct Messages from Anyone ‘, chagua kuwasha (On) kupokea ujumbe kutoka kwa mtu yeyote na zima kuzuia.
INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Hayo ndiyo maujanja ya leo kutoka Teknokona.com, tungependa kusikia kwako ungependa kujifunza nini zaidi. Kumbuka kushare kwenye mitandao ya kijamaa na marafiki yako.

Ungana nasi pia kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.