Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kuandika ujumbe

0
Sambaza

Mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza jaribio lake la kuongeza idadi ya herufi zinazotengeneza maneno katika ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwenye mtandao huo kwa mara moja hadi kufikia 280 ambayo ni mara mbili ya kiwango cha idadi ya maneno yaliyopo kwa sasa.

twitter kuongeza idadi

Twitter kuongeza idadi ya herufi katika tweet- kutoka 140 hadi 280.

Mtandao huu ambao umekuwa na idadi ya zaidi watumiaji milioni mia tatu, umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya ukuaji na hivyo inatafuta namna mbalimbali za kukuza wigo wa watumiaji.

SOMA PIA:  Uhalifu mtandao: Makosa ya mtandaoni yaliyoripotiwa kwa mwaka 2017

Kundi dogo la watumiaji wa mtandao huo watahusishwa katika jaribio hilo la kuongeza idadi ya maneno ya kuandika.

Kampuni hiyo imesema hiyo ni hatua ya kutatua moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua watumiaji wengi.

Tayari makundi mawili ya watu yamejitokeza, kuna wanaopinga mabadiliko haya na kuna walio na furaha kubwa juu ya uwezo huu. Je wewe ni mtumiaji wa Twitter? Unaonaje uwezo huu wa utakaoruhusu watu kuandika maneno mengi zaidi katika Tweet?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com