Twitter kutoondoa “Tweets” za rais Trump zinazoonekana kuwa tishio

0
Sambaza

Rais Trump ambaye amejiunga na mtandao mmoja tu wa kijamii, tweets zake nyingi zimekuwa zikitafsiriwa kama kuwa ni tishio na hivyo zinapaswa kuondolewa Twitter.

Rais Donald Trump ambaye kwa wiki kadhaa sasa amekuwa katika vita ya maneno na Rais wa Korea Kaskazini kuhusiana na majaribio ya roketi za nyuklia zenye uwezo wa kuvuka kutoka bara moja hadi jingine.

Sababu ya kutoondelewa tweets za rais Trump kwa mujibu wa Twitter ni kwamba tweets hizo zina maanufaa kwa sekta ya habari na kwa watu wote.

Watu mbalimbali wameiomba Twitter kufunga akaunti ya Twitter ya rais Donald Trump kutokana na kwamba tweets zake zinakiuka masharti ya Twiiter kwenye mtandao wake lakini Twitter imekaidi ombi hilo na kusema tweets za rais wa Marekani (Trump) hazijakiuka masharti yaliyowekwa na Twitter.

Moja ya tweets za rais Donald Trump kwa Korea ya Kaskazini.

Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii ambayo mara kwa mara inafanya mabadiliko ya masharti ambayo mtumiaji wa mtandao huo anatakiwa kuyafuata. Twitter imesema itafanya masasisho ya masharti yake kwenye Twitter na kwa tweet yoyote ile ambayo ina maslahi kwa habari na umma kwa ujumla haitaondolewa.

SOMA PIA:  Mfumo wa AI utakaoweza kufanya kazi bila intaneti unaundwa

Mapema mwaka huu ilisemekana kwamba Twitter ni mtandao ambao hautengenezi faida na vilevile inaaminika kuwa umaarufu wa mtandao wa kijamii wa Twitter unachangiwa na rais huyo wa sasa wa Marekani.

Je, unaamini kuwa umaarufu wa rais Trump unachangia Twitter iendelee kudumu mpaka leo? Usisite kutufuatilia kupitia Facebook, Twitter na hata Instagram.

Vyanzo: CNBC, Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com