Kampuni Ya Twitter Inaifanyia Majaribio Twitter Lite! #Android

0
Sambaza

Twitter Lite imeonekana huku Ufilipino na taarifa ni kwamba ipo katika majaribio. Twitter inafanya hivi ili kuhakikisha kuwa inazidi kukuwa zaidi hasa kwenye nchi zinazoendelea.

Twitter Lite ambayo imeonekana huku Ufilipino ni spesheli kwa ajili ya simu za Android pekee (bado hakuna uhakika juu ya iOS). lakini hii sio mara ya kwanza kwani mwanzoni mwa mwaka ilitoka Twitter Lite kwa ajili ya vivinjari katiika simu janja (Yaani bila ya kutumia App).

SOMA PIA:  Rihanna ajizolea karibu dola 1bn kutoka kwa Snapchat

Toleo linalotumia data kidogo tayari linapatikana kwa kuingia https://mobile.twitter.com/ kwa kutumia kivinjari (sana sana Chrome) cha simu janja yako, na kwa sasa Twitter wanaona toleo hilo liwe na app yake kabisa.

Twitter Lite

Twitter Lite Kwenye Kivinjari Katika Simu Ya Android!

Kwa Haraka Haraka Twitter Lite Ni Nini?

Ni ile Twitter ambayo imeundwa spesheli kwa ajili ya kutumika katika sehemu zenye uhaba wa intaneti ya kasi. Kwa simu  janja ambazo zina ujazo wa uhifadhi mdogo na vile vile kwa ajili ya kula sehemu ndogo ya bando la intaneti (Data).

SOMA PIA:  Jinsi ya kuzuia iOS 11 kumaliza chaji ya simu yako ndani muda mchache

Uzuri wa Twitter inayofanyiwa majaribio katika baadhi ya nchi huku katika bara la Asia ni kwamba inaweza ikafanya kazi vizuri katika simu zenye mfumo wa 2G na hata 3G.

Twitter Lite kwa ajili ya Android ina mambo mengi ambayo hata kwenye App ya kawaida iliyozoeleka yapo lakini pia kuna mengine machache ambayo yameongezwa.

Kaa mkao wa kula, kwani majaribio hayo yakifanyika vizuri Twitter Lite For Android itaanza kupatikana katika PlayStore kwa ajili ya watu wote.

SOMA PIA:  Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

Ningependa kusikia kutoka kwako, je hili mmelipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment. Je unahisi kwa mbinu hii Twitter itawafikia watu wengi?

Tembelea Mtandao Namba Moja Kwa Habari Za Teknolojia Kila SIku. Kumbuka TeknoKona Diama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com