Twitter: Sasa Utaweza Kuchati Kwa Zaidi ya Herufi 140 kwenye DM - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Twitter: Sasa Utaweza Kuchati Kwa Zaidi ya Herufi 140 kwenye DM

0
Sambaza

Katika uamuzi unaoonekana ni wa kuzidi kuwavutia watumiaji kuongeza muda zaidi katika utumiajiwa wa mtandao wao, kampuni ya Twitter umefanya mabadiliko kwa kuondoa udogo wa idadi ya nafasi kwa ajili ya kuandika ujumbe katika eneo la chati binafsi (Direct Message). Idadi hiyo itaongezwa kutoka 140 iliyo sasa, ambayo ni sawa na ile ya kuandika Tweet hadi kufikia nafasi 10,000.

go here Mabadiliko haya yatafanya watu waweze kuandikiana ujumbe mrefu zaidi katika mtandao huo bila ulazima wa kuandika na kutuma nusu nusu kama ilivyo sasa. Habari mbaya au nzuri ni kwamba mabadiliko haya ni kwa eneo la kuchati binafsi tuu, bado Tweets zitakuwa zinatakiwa zisizidi nafasi 140.Twitter

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

click Hivi karibuni kampuni hiyo imekuwa ikifanya mabadiliko mbalimbali yanayoonekana ni ya kuzidi kuufanya mtandao huo uwe bora zaidi na hivyo kuweza kuvutia watumiaji wapya wengi zaidi kuliko ilivyo sasa. Mtandao huu umejikuta hivi karibuni ukiwa na ukuaji mdogo zaidi ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii kama vile Instagram, WhatsApp, na Facebook.

Pia kampuni hiyo imeleta uwezo wa watumiaji wa mtandao huo kuweza kushirikiana katika kusambaza orodha za akaunti ambazo ni sumbufu (hii ikiwa ni zile za kutuma tuma meseji au tweets zisizokuwa salama au na maana).

Uwezo huu wa kuchati kwa maneno mengi zaidi unategemewa kuanza kusambaa taratibu kwa watumiaji na hadi kufikia katikati mwezi wa saba inategemewa utakuwa umesambaa kwa watumiaji wote wa mtandao huo.

INAYOHUSIANA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

click here Je unatumia mtandao wa Twitter? Tuambie kama mabadiliko haya ni muhimu sana kwako, je ungependa kipi kingine kifanywe na kampuni hiyo?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply