Twitter Verification: Wazi kwa wote, fuata hatua hizi!

Twitter Verification: Sasa Maombi ni wazi kwa wote, fuata hatua hizi!

0
Sambaza

Ushaangalia akaunti ya Twitter ya mtu mashuhuri au kampuni flani? Basi kwa wengi utaona kuna kialama cha vyema kimewekwa kwenye akaunti hiyo. Alama hii ambayo inahashiria ya kwamba mtumiaji ni halisi na amehakikiwa imefunguliwa kuweza patikana kwa yeyote.

Twitter verification

go Twitter Verification kama inavyoonekana katika akaunti ya Twitter inayohusu masuala yote ya ‘Twitter Verification’

buy metformin Lakini bado lazima uombe, kuna fomu ya kujaza ambayo pia itaitaji utoe sababu kwa nini ombi lako likubaliwe.

Swali mojawapo ni ‘Kwa nini ni muhimu akaunti ya muombaji ipewe sifa hiyo ya kwamba ipo ‘verified’?

here Je unataka kujua ni jinsi gani ya kufanya hivyo? Fuata hatua hizi;

INAYOHUSIANA  Google Classroom yaboreshwa

> Hakikisha

 • Hakikisha namba iliyo kwenye akaunti hiyo ya Twitter imeshahikikiwa (verified)
 • Unabarua pepe iliyohakikiwa pia
 • Kuna utambulisho kwenye profile (bio)
 • Kuna picha ya ‘Profile’
 • Kuna picha ya ‘Header’
 • Kama ni akaunti binafsi basi kuna tarehe ya kuzaliwa
 • Kuna anuani ya mtandao (website)
 • Tweets zimewekwa wazi (yaani ‘Public’ na si ‘private’

> Vingine muhimu

 • Kama akaunti ni ya mtu binafsi basi ni muhimu jina liwe jina halisi au liwe lile la kisanii
 • Kama akaunti ni ya shirika au kampuni basi jina lililo kwenye akaunti hiyo ya Twitter liwe ndilo jina rasmi linalotumika
 • Picha ya profile au header iendane kabisa na mtu au kampuni husika
 • Pia kama ni kampuni basi ata barua pepe ya akaunti hiyo iendane na kampuni husika
INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Kama umehakikisha hayo mambo yote yapo sawe basi unaweza jaza fomu ya akaunti hiyo kupitia hapa –  https://verification.twitter.com/ …Kumbuka bado Twitter wataangalia sababu za kwa nini uwe ‘verified’ na hivyo wanahaki ya kukukatalia, ila unaweza omba tena baada ya siku 30 baada ya kukataliwa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.