Twitter wakataa madai kuwa huziona nyilwa za watumiaji wa ‘Vine’

0
Sambaza

Mtandao wa kijamii wa Twitter wakanusha vikali habari ya kwamba wana uwezo wa kusoma nywila (passwords) za watumiaji wa mtandao wao wa Vine, mtandao wa kijamii unaohusisha utumaji wa video fupi.

Mtandao wa kijamii wa Vine unamilikiwa na Twitter.

Mtandao wa kijamii wa Vine unamilikiwa na Twitter.

Kwa mujibu wa OurMine(kundi linalojishughulisha na masuala ya udukuzi) lilisema kuwa liliweza kudukuwa akaunti ya Dropbox na Twitter ya Bw. Jack Dorsey(CEO wa Twitter) jambo liliongeza msukumo na kudai kuwa CEO wa Twitter anaweza kuona nyilwa za watumiaji wa mtandao ujulikanao kama ‘Vine’. Vine ilinunuliwa na Twitter mwaka 2012.

Tuliweza kudukua akaunti ya Bw. Jack na kuweza kuona vitu mbalimbali ikiweno picha iliyoko kwenye sehemu ya kurekebishia vitu  mbalimbali(control panel)  na kuweza kuona taarifa mbalimbali pamoja na passwords zao katika Vine.

Hata hivyo Twitter wamekanusha madai hayo na kusema kuwa Admin wa ‘Vine’ aliambiwa kuwa hairuhusiwi kuweza kufanya nennosiri ya mtumiaji wa mtandao huo (Vine) kuweza kuonekana katika hali yoyote ile na kuongeza kuwa passwords za watumiaji wa mtandao huo wanazitunza vizuri sana na daima zipo salama.

watumiaji wa vine

Katika mafaili ya Dropbox ya bwana Jack yaliyodukuliwa wadukuzi hao walikuta picha ya kurasa zinazoonesha mfumo wa nyuma unaotumiwa kusimamia huduma na akaunti za Vine

OurMine wameweza kudukua akaunti za mitandao ya kijamii za watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu duniani kama Mark Zuckerberg  na kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter “Tunajaribu usalama katika mtandao wako” lengo la kuu likiwa ni kufanya watu waweze kuwa na uelewa kuhusu usalama katika intaneti.

SOMA PIA:  Kampuni ya Uber yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya

Kitendo hicho cha akaunti za Bw. Jack pamoja na watu wengine maarufu duniani kudukuliwa kimezua maswali mengi na kuuliza kwanini Mkurugegenzi huyo mtendaji aliamua kuziacha taarifa mbalimbali zinazohusiana na mitandao ya kijamii wazi au hata kuzihifadhi katika ‘Dropbox?’.

Teknokona inakushauri kuwa na password ambayo ni ngumu kudukuliwa(strong password). Pia kuwa na tabia ya kubadilisha password hiyo mara kwa mara(baada ya miezi 3-6).

Soma Pia

SOMA PIA:  Nova Launcher yapakuliwa mara milioni 50 mpaka sasa

Makala hii imeandikwa kwa usaidizi wa karibu wa Tech Tines na Maine News Online

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com