Twitter: Watu wanatwiti zaidi, ila twiti zao si ndefu sana

0
Sambaza

Baada ya Twitter kuleta uwezo wa kutumia herufi 280 katika twiti moja wengi waliuponda uamuzi huo wakidai eti twiti ndefu zitaharibu Twitter waliyoizoea…lakini inaonekana hali ni tofauti. Watu wanatwiti zaidi.

Katika ripoti yao ya hivi karibuni Bwana Dorsey, Mkurugenzi wa Twitter, amesema watu wanatwiti zaidi kwa wastani kuliko kipindi cha nyumba ambapo urefu wa twiti moja ilikuwa mwisho herufi 140 tuu.

Twitter Watu wanatwiti zaidi

Twitter: Watu wanatwiti zaidi, ila twiti zao si ndefu sana

Twitter wamesema ujio wa uwezo wa kutweet twiti ndefu kuliko zamani haujaongeza wastani wa urefu wa twiti ambazo watumiaji wake wanatwiti katika mtandao huo.

Ila wameona muongezeko wa mazungumzo (engagement), hii ikiwa ni pamoja na ongezeko la wastani wa Retweets, na Mentions. Pia kuna ongezeko la utengenezaji wa urafiki kupitia ‘Followers’.

SOMA PIA:  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Ingawa mambo ni mzuri kwa ujumla wake ila mambo si mazuri sana kwa soko la Marekani. Katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka Januari 2016 hadi Januari 2017 Twitter kwa wastani watumiaji wa kila mwezi wa mtandao huu wa kijamii wamepungua kutoka wastani wa watumiaji milioni 69 kwa mwezi hadi watumiaji milioni 68.

Je wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Twitter? Unaona uwezo wa kutwiti herufi 280 umepafanya Twitter sehemu nzuri zaidi.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com