Twitter yafanya maboresho katika namna ya ku-tweet

1
Sambaza

Mtandao  wa The Verge umeripoti kwamba tarehe 19/09/2016 Twitter itafanya maboresho mengine ambayo tayari yalikwisha tangazwa mwezi Mei, pamoja na yote mtandao huu sasa hautahesabia viambatanisho vilivyo ndani ya tweet katika hesabu ya tarakimu 140.

tweet

kwa sasa majina, picha, video, GIF ama link hazitahesabiwa katika tarakimu 140 ambazo mtu anaruhusiwa kutumia katika tweet moja, maboresho haya yanalenga katika kuwaruhusu watumiaji kujieleza kwa urahisi zaidi katika mtandao huu.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba @Twitter wameongeza uwezo wa watu kuandika tweets kwa kuondoa viambatanisho kama picha video GIF na vinginevyo katika hesabu ya tarakimu 140, hii inamaanisha kwamba sasa tunaweza kushiriki mijadala mbalimbali kwa ufasaha bila kujibana.

SOMA PIA:  Samsung: Ukiwa na monitor hii uchezaji magemu utakuwa muruwa zaidi

Yafuatayo ni mabadiliko mengine ambayo yanatarajiwa kuja mwezi huu…….

1. .@ Kwa sasa haitatumika tena!

Sio kila mtu alikuwa anaijua na kuitumia hii .@ ????(mimi ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawaitumii) ni kwamba kwa sasa ukiandika tweets ukaanzia na jina la mtumiaji mfano @Teknokona basi tweet hii itamfikia @Teknokona pekee ila wanaokufuata hawataiona ilikua ukitaka wengine waione basi lazima uanze na nukta.

Twitter wanataka kubadili hili hivyo siku zijazo Tweets zote zinazo anza na jina la mtumiaji zitaweza kuwafikia watu wote wanaomfuata mtumiaji.

SOMA PIA:  IFA 2017 kufanyika kuanzia Septemba 1-6 jijini Berlin

2. Majina pia hayata hesabiwa!

Kwa sasa ukitweet basi majina ya wale ambao unawapelekea ujumbe huo pia yanahesabiwa, hili ni moja kati ya mambo ambayo yatabadilishwa mwezi huu na hivyo majina yatakuwa hayahesabiwi.

Tayari Twitter wamekwisha leta uwezo wa mtumiaji kuretweet tweets zake mwenyewe kitu ambacho waliahidi pia mwezi Mei, ingawa bado haijulikani ni lini mabadiliko haya yatawafikia watumiaji wa kawaida hasa kwa Afrika lakini ni taarifa njema kwa watumiaji ambao wamekuwa wanakerwa na sheria ya tarakimu 140

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.
error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com