Unakumbuka idadi ya herufi ambazo Twitter ilikuwa ikiruhusu kwaenye jina la akaunti ya Twitter? Unaweza usiwe unakumbuka au hata kufahamu kutokana na ukweli usipingika kuwa si watu wengi wanatumia wamejiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter.
Ni miezi michache tu Twitter ilitangaza uamuzi wake wa kuongeza idadi ya mameno kutoka jumla ya maneno 140 kwa tweet noja na kuwa mara mbili yake (maneno 280) kwa tweet moja. Na sasa inaonekana ni zamu ya kuongeza idadi ya herufi za jina linaloonekana kwenye profile ya mhusika.
Awali Twitter iliruhusu herufi za majina zisizozidi ishirini (20) kwenye jina la akaunti la mtumiaji wa Twitter na sasa imeamua kuongeza mpaka herufi 50.
Hii ina maana ya kwamba jina ulatumia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter unaweza ukaongezea jina la katikati, ukoo, jina lako maarufu, n.k na kama ukitaka kuliremba zaidi unaweza ukaongezea na emoji ili mradi tu maneno yote kwenye jina hilo yasizidi herufi/alama maalum hamsini.
Uwezo wa kuhariri jina la linaloonekana kwenye akaunti yako ya Twitter unaweza kufanya kupitia kwenye app ya Twitter au hata kupitia kwenye tovuti yao (Twitter) kwa kuingia kwenye profile yako kisha unaenda kwenye edit profile kubadilisha jina lako upendavyo.
Twitter haijaazia kwenye jina tu bali ilishaleta mambo kadhaa kuvutia mtandao huo wa kijamii. Umelipokeaje suala zima la Twtter kuamua kuongeza idadi ya herufi za jina la mhusika kwenye mtandao wa kujamii wa Twitter?
Vyanzo: Gadgets 360, BGR India, Marshable
One Comment
Comments are closed.