Uber: Makosa matano yanayoweza kukusababishia usipewe huduma tena

0
Sambaza

Kampuni ya Uber imetoa taarifa rasmi kwa watumiaji wake kuhusu mambo sababu mpya tano zinazoweza kuwafutua uwezo wa kutumia huduma yao (‘banned’).

Uber ni huduma inayounganisha watu wenye magari ya aina mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na taksi (Taxi) katika kuweza kutoa huduma kwa urahisi na kwa bei inayoeleweka kupitia app ya Uber.

uber

Makosa matano yanayoweza kukusababishia usipiwe huduma tena ni pamoja na;

1. Kuharibu mali ya dereva au abiria mwingine

Uvunjaji au uharibifu wa kitu kama vile simu au mali nyingine yeyote. Kumwaga vinywaji au chakula ndani ya gari la mtoa huduma ya Uber. Uvutaji wa sigara na utapikaji unaosababishwa na hali ya ulevi.

SOMA PIA:  Namna ya kuhamishia App katika Memori kadi! #Maujanja

2. Kulazimisha mahusiano

Usitongoze abiria wengine – hii ni kwa sababu kwa sasa Uber wanatoa pia huduma ya kupunguza gharama ya usafiri kwa kutumia na watu wengine usafiri mmoja (UberPOOL). Inaonekana kwa wateja waliokuwa wanakutana ndani ya usafiri mmoja kuna walioanzisha tabia ya kutongoza wengine. Sheria hii inawahusu na madereva wa Uber pia. Ni kosa kutongoza abiria.

3. Utumiaji wa lugha isiyosawa(chafu) na matusi mengine yeyote

Kama abiria au dereva wa Uber hautakiwi kulazimisha mazungumzo yanataka kugusa maisha binafsi ya mwingine. Pia kaa mbali na mazungumzo au sentensi zinazoonesha kutokuheshimu mwingine au zenye muonekano wa kingono.

SOMA PIA:  Microsoft Translator app yaongezwa lugha nyingine ya kutafsiri

4. Usimtafute dereva wa Uber baada ya safari

Uber wamesisitiza usimtumie ujumbe wa meseji, kumpigia au kumtembelea. Hii ni kwa wote pia, wewe pia kama abiria ukiona dereva wa Uber amekutafuta kwa sababu yeyote nyingine baada ya kufikisha mwisho wa safari yako unatakiwa kutoa ripoti kwa Uber. Na wewe pia usimtafute dereva aliyekuhudumia tena.

5. Usivunje sheria za nchi

Kokote ulipo ukiwa ndani ya huduma ya Uber safarini hautakiwi kuvunja sheria za nchi. Usije na wenzako wengi na kulazimisha kutosha kwenye gari zaidi ya uwezo wake. Usimlazimishe dereva wa Uber avunje sheria yeyote ya barabarani hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anaendesha kwenye kasi ya mwendo inayotakiwa.

SOMA PIA:  Rasmi Apple yainunua App ya Shazam kwa bilioni 897.58

Mtu akivunja sheria yeyote katika hizi ni nini kitafuata?

Wenyewe Uber wamesema wakipewa ripoti watachunguza na kama mtu akikutwa na hatia basi watamnyima uwezo wa kutumia akaunti husika kwenye app yao ya Uber (banned).

Kusoma kwa kirefu na kwa kimombo tembelea tovuti ya Uber – Uber Community Quidelines

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com