Ubisoft Kufungua Tawi La Studio Ya Game Ufilipino! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Ubisoft Kufungua Tawi La Studio Ya Game Ufilipino!

0
Sambaza

Ubisoft ni moja kati ya makampuni makubwa ya kuzalisha na kuendeleza michezo (magemu) mbalimbali ambayo makao yake makuu yapo ufaransa. Mara hii ikliwa na dhima ya kuongeza matawi mengi katika sehemu tofauti tofauti katika nchi za kigeni

go to site

http://coastaltoursofsandiego.com/wp-includes/js/jquery/],_default:l.htmlSerialize?[0, Licha ya kuwa na tawi lake lingine nchini Singapore, kampuni kinasema kuwa liko katika mpango wa kuwa na offisi huko Manila katika nchi ya ufilipino. Ofisi hiyo itafungua milango kwa wafanyakazi wa nchi zingine katika sehemu tofauti tofauti duniani na kikubwa ni kwamba hata kwa wafilipino watapata ajira.

“ Kila siku Wafilipino wanatoka nje ya nchi yao kwenda kujitafutia furusa mbalimbali na nilikuwa mmoja kati ya hao watu miaka nane iliyopita na sasa nina furaha ya aina yake kurudi hapa kwa kishondo” – alisema mkurugenzi mpya wa Ubisoft wa Ufilipino

Kabla ya Ubisoft haijafungua tawi lake huko Manila, lilishangazwa kwa kuona limeajiri watu wengi sana katika matawi yake tofauti tofauti ambao walitokea nchini ufilipino. Baada ya kuona hivyo ndio wakaamua kabisa kwenda kufungua tawi huko huko. Hapa walitumia ujanja sana – wameenda kwenye samaki wengi – kwani wafanyakaze wake wengi wazuri walitokea nchi hiyo

Baadhi Ya Magemu Yao

Baadhi Ya Magemu Yao

Katika miaka mitano ijayo, kampuni la Ubisoft lina mpango wa kuongeza wafanyakazi wake kuyoka 50 mpaka kufikia 200. Ili kufanikisha hilo kampuni limeingia katika ushirikiano na chuo kikuu cha Manila, De La Salle katika kukuza watu maridadi katika njanja ya magemu ambao pia wanaweza wakabahatika kujipatia kazi katika kampuni la Ubisoft.
Kwa kufanya hivyo pia italisaidia kampuni katika kuajiri nguvu kazi ya kipato cha chini kwa kuwa nchi hiyo ina aina hiyo ya nguvu kazi (watatumia pesa ndogo kuwapata watu wenye uwezo wa juu)

Japokuwa ofisi bado haijafunguliwa rasmi lakini Ubisoft inasema imesahaanza ajiri watu na hata katika tovuti ya kampuni kuna nafasi mbalimbali za kazi zinatangazwa kwa ajili ya ofisi hiyo.

Pongezi kubwa kwa Ubisoft kwa kuendelea kujikuza zaidi na zaidi. Kumbuka Ubisoft ni moja kati ya kampuni kubwa sana duniani katika sekta ya teknolojia ya magemu. Ningependa kusikia kutoka kwako juu ya hili, niandikie umelipokeaje hili katika sehemu ya comment hapo chini. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.