Kivinjari cha UC Browser chaondolewa katika soko la Apps la Google PlayStore

0
Sambaza

Moja ya kivinjari bora na maarufu kwa watumiaji duniani wanaotumia simu za Android cha UC Browser chaondolewa katika soko la apps la Google PlayStore.

Kivinjari cha UC Browser kinatengenezwa na kampuni maarufu ya nchini Uchina, Alibaba.

Kabla ya kuondolewa kwake kwenye soko la PlayStore app hii ilikuwa imeshushwa zaidi ya mara milioni 500 kufikia mwezi uliopita. Inawatumiaji wengi duniani kote, hasa hasa kwa wanaotaka kutumia kiwango kidogo cha data. Mfano kwa nchini India tuu app hiyo ina watumiaji zaidi ya milioni 100.

SOMA PIA:  Huduma ya WhatsApp ilivyopotea jana usiku katika mataifa mengi

app uc browser

Ingawa app ya UC Browser imeondolewa bado kuna apps zingine ambazo hazijaondolewa na Google, na zinazotengenezwa na kitengo hicho hicho cha Alibaba – UC Web. Apps hizo ni pamoja na UC Browser Mini (toleo dogo la UC Browser).

Je ni kwa nini Google wameiondoa UC Browser katika soko lake la apps?

Watafiti wanaona kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu kadhaa. Ni hivi karibuni tuu app hiyo ilishatuhumiwa kuhusika na kutuma data za watumiaji wake wa nchini India kwenda kwenye server zao nchini China – hili ni hatari kwa usalama wa data za watumiaji.

SOMA PIA:  Instagram yazidi kuiiga Snapchat, yaleta face filters na Hashtags

Ila habari za uhakika zinaonesha Google wamechukua hatua ya kuondoa app hiyo na kuipa siku saba za kujichunguza na kuomba kurudishwa kutokana na kosa la kuonekana kuongeza downloads zake kwa kutumia njia zisizohalali.

UC Browser chaondolewa katika soko la Apps

Utumiaji wa UC Browser Tanzania – Oktoba 2016 – Oktoba 2017

Utumiaji wa kivinjari cha UC Browser umekuwa na ukuwaji wa taratibu nchini Tanzania. Kwa sasa app hiyo ni ya tatu, ikichukua asilimia 19.17 ya watumiaji wote wa vifaa vya simu, nyuma ya Opera (asilimia 42.08) na Chrome (asilimia 23.69).

Adhabu ya Google inaweza dumu kwa siku 7 hadi siku 30 kulingana na uharaka wa UC Web kurekebisha njia zake za kujitangaza. Ila kwa sasa unaweza kwenda kwenye tovuti yao na kudownload file la app hiyo – UC Web

SOMA PIA:  Udukuzi kwenye Instagram; Akaunti za watu maarufu zaingiliwa!

Soma pia – Jinsi ya kudownload na kuinstall app nje ya Google PlayStore

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com