Udanganyifu unaoweza kusababisa ‘ukaibiwa kidigitali’ wabainika kwenye bidhaa za Apple

0
Sambaza

Tunapozungumzia bidhaa ambazo zinaaminika kuwa ni salama kutokana na ulinzi ulionao hatuwezi kuacha kutaja bidhaa za Apple kwenye orodha ingawa si kwamba bidhaa hizo hazina udhaifu.

Hivi karibuni katika mataifa mengi ulimwenguni kwa watumiaji wa bidhaa zinazotengenezwa na Apple wamekumbana na kasumba ambayo inaweza kusababisha wakaibiwa pesa zao kidigitali. Na sasa watumiaji wametaarifiwa kuwa makini na taarifa fupi (notifications) wanazoweza kupata kwenye vifaa vyao (simu, kompyuta, iPod, iPad, n.k).

Mfano wa taarifa fupi ya kweli na ya uongo.

Namna ambavyo mtu anaweza kaingia kwenye mtego wa kuibiwa kwenye vifaa vya Apple.

Udanganyifu huo umelenga kufanyika katika hali ya kawaida kabisa pale ambapo unaperuzi huku na kule kwenye simu janaja yako aina ya iPhone, Ipad au kompyuta kutoka familia ya Mac, n.k. Ghafla tu unashangaa inatokea taarifa fupi (notification) ikikuomba uweke taarifa zako za siri za kwenye simu yako, Apple ID na nywila.

Picha ya upande wa kushoto ni nototfication ya kweli. Picha ya pili ni notification ya uongo yenye lengo la kupata taarifa zako njia unayotumia kufanya malipo kwa njia ya kielekroniki.

Si jambo rahisi kubaini kuwa taarifa fulani si ya kweli hivyo usiopkuwa makini na ukakubali kudanganyika na ukaweka taarifa zako za siri (Apple ID na password) utakuwa umeruhusu mhusika (aliyetuma taarifa) kuweza kukuibia kiasi ambacho atapenda yeye.

Kwa benki kubaini kuwa muamala fulani ulifanyika si wa kweli inaweza kuchukua muda. Na hata ikija kubainika inaweza ikawa ni vigumu/isiwezekanane kabisa kurudishiwa kiasi ulichoibiwa/kilichochukuliwa bila idhini yako.

Namna ya kuujua udanganyifu huo na jinsi ya kuuepuka.

Taarifa fupi inayotokea kwenye vifaa vya Apple ikidai uweke Apple ID yako na nywila (password) lazima kile kimstari itakuwa kinatokea na kupotea, kama haifanyi hivyo basi ujue na kutambua kuwa taaria hiyo si ya kweli. Pili, kama ukitoka/ukifunga app ulyopo na kisha ile notification pia ikatoka basi ujue taarifa hiyo ilikuwa ni ya uongo. Ili kuepukana na kadhia hiyo ni kutoka kabisa kwenye sehemu uliyopo na kuingia Settings kisha kuweka Apple ID na nywila (iwapo notification ni ya kweli).

Picha ya upande wa kushoto: Neno “Loading” rangi yake haijakolea (taarifa ya kweli). Picha ya upande wa kulia: Neno “Loading” rangi yake imekolea na maandishi yake ni makubwa (taarifa ya uongo).

Taarifa za uongo kwa upande wa teknolojia zimekuwa ni jambo ambalo si la kushangaza sana siku hizi lakini sasa  wajanja wachache wameamua kuhamia kwenye simu janja kaama uwanja mpya wa kutekeleza mabaya yao.

Usisite kutuuliza TeknoKona pale unapohisi kitu cha kutia mashaka kwenye simu/kifaa chako. Je, una maoni? Tuandikie maoni yako hapo chini.

Vyanzo: The news in color, Felix Krause

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Tetesi: Gharama ya iPhone 8 kuwa zaidi ya sh. 2.2M
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com