UDART: Sasa unaweza kuongeza salio kwa M-PESA - TeknoKona Teknolojia Tanzania

UDART: Sasa unaweza kuongeza salio kwa M-PESA

0
Sambaza

Watumiaji wa usafiri wa mabasi ya umma ya UDART sasa wataweza kuongeza pesa katika kadi zao kwa kupitia M-PESA, Vodacom inakuwa ndiyo kampuni ya kwanza ya simu kuwapatia wateja wake uwezo wa kuongeza pesa katika kadi za kusafiria katika mabasi haya ya UDART.

http://murphy1chiro.com/massage-therapy/

kadi udart

enter site Kadi zinazotumika katika usafiri huo wa UDA

click here UDART walitangaza kusitisha tiketi za karatasi na hivyo kuhimiza watumiaji wa usafiri huu mpya kununua kadi ambazo ndizo pekee zitatumika, hatua hii iliacha changamoto moja tu kwamba kuongeza pesa katika kadi ama kujua kiasi cha pesa kilichobaki katika kadi yako ilikubidi kupanga foleni katika kituo kitu ambacho hakikuwa kizuri sana kwa watumiaji.

13423429_1016037351828323_1825959119_n

Basi la UDART likiwa katika moja ya safari yake.

Vodacom wameliona hilo na kuamua kuleta huduma ya M-PESA kwa wateja wake ambao wanatumia UDART, kuanzia sasa wateja wa Vodacom hawatahitaji kukaa foleni kusubiri kuongeza salio katika kadi zao UDA bali wataweza kufanya hivyo kwa kutumia M-PESA.

INAYOHUSIANA  Programu tumishi kutoka kwa msanii wa Tanzania

Kuongeza salio katika kadi yako ya UDA fuata hatua zifuatazo:-

  1. Piga *150*00# chagua LIPA KWA M-PESA,
  2. Chagua DART,
  3. Weka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba ya kadi yako ya DART,
  4. Weka KIASI (Mfano 2000, 5000, 10000 n.k),
  5. Weka PIN yako ya M-Pesa,
  6. Bonyeza 1 kukamilisha muamala.

Utapokea ujumbe mfupi kuthibitsha muamala wako.

Tunategemea mazungumzo yanafanywa ilki kuwaruhusu watumiaji wa mitandao mingine pia kuweza kuongeza salio kwa kutumia mitandao yao, pia ni tumaini la wengi kwamba sasa tutaweza kuanza kuangalia salio katika kadi zetu kwa kutumia simu pia ili kuondoa usumbufu.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.