Uhalifu mtandao: Makosa ya mtandaoni yaliyoripotiwa kwa mwaka 2017 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Uhalifu mtandao: Makosa ya mtandaoni yaliyoripotiwa kwa mwaka 2017

0
Sambaza

Uhalifu wa mtandao ni uhalifu unaoshika kasi duniani katika miaka ya karibuni. Hii imetokana na ukuaji wa teknolojia ambapo mambo mengi yamerahisishwa kiutendaji.

http://acl-tx.com/plans/life-term/?Show Agent Q=2 Kukua kwa teknolojia, kumetoa pia nafasi kwa wahalifu kubuni mbinu mpya kila wakati ili kufanikisha matukio ya kiuhalifu. Takwimu zinaonesha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Juni mwaka 2017, kumeripotiwa makosa ya mtandao 3,346 nchini, huku wilaya ya Kinondoni ikiongoza kwa kuwa na makosa 1,383.

wadukuzi wa mtandao Uhalifu mtandao

go Watu wengi wamekuwa wakifanya makosa ya kimtandao kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya teknolojia ama kuwa na uelewa mdogo wa sheria za makosa ya mtandao pamoja na mabadiliko yanayotokana na kukua kwa teknolojia.

Mpaka mwishoni wa mwezi Novemba zaidi ya makosa ya mtandaoni 7,900 yaliripotiwa. Mwaka 2016, zaidi ya makosa 8,700 yaliripotiwa huku zaidi ya makosa 7,700 yakipelekwa mahakamani.

Makosa ya mtadao yanajumisha:-

see url kusambaza taarifa za uongo, kuingilia mawasiliano ya mtu bila ridhaa yake, kusambaza na kumiliki picha za ngono za watoto, kusambaza picha za utupu, uchochezi, kuzidisha muda wa kubakia kwenye mfumo wa kompyuta pamoja na kutuma meseji za uchochezi, n.k.

Kwa sasa asilimia 90 ya makosa yanayofanyika yanahusisha teknolojia ya kompyuta na mawasiliano.

Makosa mengine ni kuzuia upelelezi, kuingilia data kinyume cha sheria, ujasusi wa data, ufichuaji wa taarifa za upelelezi, kughushi kunakohusiana na kompyuta, udanganyifu unaohusiana na kompyuta pamoja na wizi wa haki miliki.

Ni vema kuwa na utaratibu wa kubadilisha namba za siri mara kwa mara ili kuepuka wahalifu kukariri namba yako na kuepuka kutumia namba ya siri moja kwa akaunti zaidi ya moja.

Kuweka namba za siri kwenye vifaa vya ki-elektroniki unavyovitumia itakuepusha na vitendo vya kihalifu dhidi ya vifaa vyako ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vifaa vyako vya mawasiliano unavyotumia vina ubora na sio bora kifaa.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.