Ujenzi wa Darubini kubwa zaidi duniani waanza. - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Ujenzi wa Darubini kubwa zaidi duniani waanza.

0
Sambaza

Umoja wa mambo ya anga wa Ulaya umeanza ujenzi wa darubini ambayo ikikamilika itakuwa ndiyo darubini kubwa zaidi. Ujenzi wa darubini hii unategemewa kusaidia harakati za ugunduzi wa anga hasa sayari mpya na maisha katika sayari hizo.

http://passionistvolunteers.org/meet-our-volun…

watch

go site Darubii hiyo ambayo imepewa jina la European Extremely Large Telescope inajengwa katika mlima wenye urefu wa mita 3000 katika jangwa la Chile. Ujenzi huu utakapokamilika  darubini hii itakua ni mara tano zaidi ya darubini kubwa zaidi sasa hivi.

Ujenzi wa darubini hii unategemewa kukamilika hapo mwaka 2024 ambapo sio tu kwamba itakuwa ndiyo darubini kubwa zaidi duniani pia itakuwa inawezakukusanya mwanga mara 13 zaidi ya darubini zilizopo kwa sasa.

INAYOHUSIANA  Bios Cube: Majivu ya marehemu kutumika kukuza mmea

Darubini hii inajengwa na umoja unaoundwa na nchi mbalimbali zikiwamo Brazil Ujerumani Uingereza na Ufaransa, Mkurugenzi mkuu  wa umoja huo amesema kwamba ujenzi wa darubini hii ni hatua kubwa katika sayansi ya anga kama ilivyokuwa kwa ugunduzi wa darubini ya kwanza ya mwanaanga Galileo.

Uzinduzi wa ujenzi wa Darubini hii ulifanywa na raisi wa Chile Bi Michelle Bachelet amesema ujenzi wa darubini hii ni kielelezo tosha cha nguvu ya ushirikiano wa kimataifa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.