Programu endeshaji ya iOS 11 iliyoboreshwa zaidi kwenye bidhaa za Apple - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Programu endeshaji ya iOS 11 iliyoboreshwa zaidi kwenye bidhaa za Apple

1
Sambaza

Ile tabia ambayo Apple wamekuwa nayo tangu Sept 2016 inategemewa kujirudia tena kwani wengi wetu tunajua kuwa iPhone 8 ipo njiani kuja lakini swali ni je, itakuja na iOS 11 ileile iliyotoka siku 3 kabla ya iPhone 7 kupelekwa sokoni?

Kwa kuwakumbusha tu wasomaji wetu ni kwamba http://bestfriendborrowed.com/tag/articles/ iOS 11 si ngeni kwenye soko na kwa mara ya kwanza ilitoka Sept 13 2016 na siku 3 tatu baadae iPhone 7 ikawekwa sokoni. Programu endeshaji yenye jina sawa na lile la mwaka 2016 inatarajiwa kutoka hivi karibuni na kuna uvumi kuwa iPhone 7s, 7s plus na iPhone 8 ziitakuja zikiwa na iOS 11 iliyoboreshwa zaidi.

Muonekano wa mbele kwenye iOS 11.

Ni vitu gani vimeongezwa kwenye iOS 11?

Apple wanasifika kwa kutengeneza vitu vyenye mvuto wa aina yake na katika iOS 11 wataleta kitu kinachoitwa “Peer-to-peer Apple pay“. Mfumo wa peer-to-peer unawezeshwa na iMessage kwa maana ya kwamba mtu ataweza kufanya miamala ya kipesa kupitia iMessage (haitahusisha miamala kama TigoPesa, Mpesa, Airtel money, n.k) ila itahusisha malilpo ya Credit card, Debit card, n.k.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe

http://castlerockelectricalcontractor.com/how-to-choose-an-electrical-contractor/ Pia itakuwa iliboreshwa sana kwenye upande wa kuweza kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Upande wa kamera nao haujaachwa nyuma kwwani kwenye toleo hilo la programu endeshaji kamera itakuwa imeboreshwa vilivyo.

Umewahi kufikiria Apple kukuangusha tunapozungumzia unapopatwa na dharura au unahitaji usaidizi fulani kutoka kwenye simu yako? La hasha! Basi iOS 11 itakuwa na vitu vilivyoboreshwa zaidi kama programu tumishi ya Siri pamoja upande wa dharura, tazama picha:

 iOS 11 iliyoboreshwa

Pale utakapotaka kubonyeza kitufe cha kuzima simu au kama unataka kupiga namba ya dharura basi huo ndio muonekano wake kwenye iOS 11 mpya.

Muonekano wa app ya Siri kwenye iOS 11 iliyoboreshwa

Katika masuala mengi duniani kuachana na vitu fulani na kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ni jambo ambalo limezoeleka hasa kwa wale wanaotumia vifaa vya “Kileo”. Basi vivyo hivyo si bidhaa zote za Apple zitakavweza kufanya masasisho na kuweza kutumia iOS 11 iliyoboreshwa.

INAYOHUSIANA  Piga simu kwa watu wengi kwa njia ya WhatsApp

http://deirdreverne.com/news/page/13/?s= Bidhaa za Apple zitakazonufaika na ujio wa iOS 11

  • iPhone: 5s, 6, 6 Plus, 6s, 6s Plus, SE, 7, 7 Plus
  • iPad: Kizazi cha 5 (2017); Mini 2, 3 and 4; pamoja na matoleo yote ya iPad Air na iPad Pro
  • iPod Touch: Kizazi cha 6 (2015)

iPhone 5, 5c na iPad 4 ya mwaka 2012 ni moja kati ya vifaa ambavyo havitaweza kupokea masasiho na kuweza kutumia iOS 11. Kama wewe unatumia iPhone 5s na kuendelea mara tu itakapozinduliwa na kuanza kutumia ingia Settings -> General -> Software Update.

Vyanzo: Telegraph, The verge

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|