Mambo 20 Kuhusu Mtandao Wa Kijamii Wa Twitter!

0
Sambaza

 

twitter-t8t9jj-520x245

http://candacenkoth.com/?q=viagra-5mg-daily-dose Twitter ni mtandao wa kijamii wa pili kwa ukubwa duniani. Maarufu kwa meseji zake zenye maneno 140 tuu zinazojulikana kama ‘Tweets’. Twitter ilianzishwa mwezi  Machi 2006 na katika kipindi cha miaka nane ilipata umaarufu wake duniani kote. Kwa sasa Twitter ina watumiaji zaidi ya milioni 271 ambao wako hai (active users), amabao wana Tweet Tweet milioni 500 kwa siku kwa kiwango cha  Tweet 1,40,000 kwa sekunde. Inavutia Sio?

 

 1. Jina la mwanzo la twitter lilikua ni ‘Twttr’ amabalo baadae lilibadilishwa na kuitwa ‘Twitter’.
 2. Hivi sasa ina watumiaji milioni 271 ambao wako aktive kila mwezi na watumiaji  milioni 974 ambao wamejisajili. Kati ya hizo akaunti milioni 20 ni feki
 3. Inasemekana  tweets 1,40,000  zinatumwa kwa sekunde na tweets  milioni 500 kwa siku
 4. 44% ya akauti zilizosajiliwa kati ya zile 974 hazipost kitu twitter na 40% ya akaunti za twitter wamejisajili kuangalia habari tuu
 5. Neno ‘Love’ ndio linatumia sana kwenye bio za watu
 6. Twitter ilipata tweet yake ya kwanza Machi 21, 2006. Twitter ilikua inasema “Just setting up my twttr” . Na unafikiri mtu gani wa kwanza kutuma tweet ya kwanza? Umepatia!! Ni Jack Dorsey, mwanzilisha wa Twitter alituma hivyo
 7. Ilichukua miaka 3 miezi 2 na siku 1 Twitter kufikisha Tweet Bilioni. Wakati siku hizi inachukua wiki watumiaji wa Twitter kutuma Tweets bilioni
 8. Hivi unjaua ni tweet gani iliyopata tweets nyingi? Hujui!! Ni Hii hapa Tweet Ya Barack Obama (@BarackObama). Tweet ya ushindi iliyopata zaidi ya Tweet 800,000 Na hiyo tweet ilikua inasema “Four more years”.
 9. 80% ya viongozi duniania wanatumia twitter na kiongozi maarufu zaidi ni Raisi wa Marekani, Barack Obama
 10. Michezo ya Olympiki iliyofanyika London mwaka 2012 ilitoa zaidi ya tweet milioni 150 Twitter
 11. Unaweza usijue lakini nchi ya Sweden ina akaunti twitter (@Sweden).  Na inafanya kazi kirahisi tuu, ina muachia mamlaka raia yeyote wa sweden ambae anatka kuitumia akaunti hiyo kwa mda wa wiki moja tuu. Huyo mtu mmoja ambae anaeachiwa acount hiyo kwa wiki nzima ana uhuru wa kubadilisha bio na picha na kutweet kitu chochote anachotaka
 12. Adam Parrish alifungua Akaunti twitter (@Everyword). Akaunti hii inmetweet Kila neno ya kiingereza katika kamusi ya kiingereza. Mpaka sasa imetweet zaidi ya tweet 1,000,00 kila moja ikiwa na neno moja tuu. Kazi ya kutweet Kila neno halisi ya Kiingereza ilianza mwaka 2007 na imeisha mwaka 2014
 13. Ushawahi waza jinsi vita kuu ya pili ya dunia jinsi ilivyokua? na unegependa kuona kidogo yaliyojiri?. Njia mbadala ni hii hapa. Alwyn Collinson, Mwanahistoria wa Oxford alianzisha akaunti ya vita kuu ya dunia ya pili twitter (@RealTimeWWII). Hivi sasa Akaunti hiyo ina zaidi ya Tweet 6600 na zaidi ya followers 300000
 14. Novemba 2011 Twitter ilichukua uamuzi wa kishujaa kwa kukata Facebook kuinunua kwa dola za kimarikani 500. Kwa muda huo twitter ilikua na watu milioni 6 tuu waliojiandikisha. Mpaka sasa twitter ina zaidi ya watumiaji milioni 974 na sasa twitter ina thamani ya dola za kimarekani bilioni 11
 15. Mwaka 2009 Auston Kutcher (@aplusk), wa marekani alikua mwigizaji wa kwanza kuwa na followers zaidi ya milioni moja. hivi sasa anao followers milioni 16.5
 16. Mwezi machi 2009. Mtaalamu wa anga Mike Massimino (@astro_mike) alituma Tweet ya kwanza kabisa kutoka juu ya anga. Tweet ilikuwa ikisema “From orbit: Launch was awesome!! I am feeling great, working hard, & enjoying the magnificent views, the adventure of a lifetime has begun”.
 17. Unamjua James Cameron(@JimCameron)? Hapana? Ni Mtu wa kwanza kutuma tweet chini ya kina kirefu cha maji duniani. Sehemu ni Mariana Trench katika bahari ya pasifiki. Tweet ilisema “Just arrived at the ocean’s deepest pt. Hitting bottom never felt so good. Can’t wait to share what I’m seeing w/ you
 18. Mwezi Mei 2011. Mwana IT wa pakistani Sohaib Athar (@ReallyVirtual) alitweet hivi “Helicopter hovering above Abbottabad at 1AM(is a rare event).”  bila kujua alivuja taarifa za uvamizi wa Majeshi ya marekani katika nyumba ya Osama Bin Laden kabla ya chombo chochote cha habari. Osma Bin Laden aliuwawa katika oparesheni hiyo.
 19. Mtu Maarufu kuwa na followers wengi twitter katika historia ni katy perry (@katyperry), ana followers zaidi ya milioni 58.6.  Ana followers wengi zaidi ya umati wa watu wa Ujerumani, Afrika ya Kusini, Turkey, Canada, Egypt na Ajentina.
 20. Hivi unamjua mtumiaji wa twitter amabae anafollow watumiaji wengi zaidi?  Ni huyu hapa ArabicBest (@ArabicBest). Anafollow watu milioni 2.42 twitter.
Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Ujenzi wa betri kubwa kuliko yote mpaka sasa wakamilika kwa 50%
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com