Umoja wa Ulaya kuipiga faini Facebook kutokana na utumiaji wa data za WhatsApp

0
Sambaza

Umoja wa Ulaya kuipiga faini Facebook. Bodi ya usimamiaji wa ushindani barani Ulaya, Chini ya Umoja wa Ulaya (EU) limewatia hatiani Facebook kwa kosa la kuwadanganya katika hatua za uchunguzi uliowapa ruhusa ya kununua WhatsApp.

Katika moja ya hatua zilizohakikisha Umoja wa Ulaya unatoa ruhusa kwa Facebook kukamilisha ununuaji wake wa huduma ya WhatsApp ilikuwa ni kigezo cha wao kuwaambia wazi ni jinsi gani wataendelea kutumia data za watumiaji wa huduma hiyo. Kipindi wanapewa ruhusa walidai hawana uwezo wa kuunganisha taarifa na kuwatambua watumiaji wa WhatsApp na Facebook kupitia taarifa za kidata…lakini hili wameweza lifanya kwa sasa.

Mwezi wa 8 mwaka 2014 Facebook waliiambia bodi hiyo ya Ulaya kwamba haiwezekani kabisa kuunganisha taarifa ya mtumiaji mmoja wa WhatsApp na akaunti yake iliyo Facebook – hili ni jambo ambalo lilichangia wao kupewa ruhusa ya kuinunua WhatsApp… Ila miezi michache iliyopita walikuja na mabadiliko WhatsApp yanayotuma data za WhatsApp kwenda Facebook.

SOMA PIA:  BrighterMonday Yaleta Mapinduzi Katika Soko La Ajira Tanzania!

Kwa kiasi kikubwa chombo cha masuala ya kibiashara cha Umoja wa Ulaya kinaona Facebook walificha uwezo huo kipindi kile kwani waliogopa kama chombo hicho kingefahamu basi ununuzi wao wa WhatsApp ungepingwa katika bara la Ulaya.

Ulaya kuipiga faini Facebook

Bodi hiyo ya biashara ya bara la Ulaya imesema Facebook walitoa taarifa ‘zisizokuwa za ukweli/yaani uongo’ katika kipindi cha uchunguzi ambao ulifanyika ili kujiridhisha ununuaji wa WhatsApp usingeleta madhara kwa watumiaji wa huduma hiyo.

Soma pia:

Facebook wamepewa hadi Januari 31 kujitetea, kama bodi hiyo haitajridhika na majibu basi Facebook watapigwa faini ya asilimia 1 ya mapato yao yote duniani kote.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com