Umiliki wa Intaneti; Sasa wa Kimataifa na si Marekani pekee!

0
Sambaza

Kuna mabadiliko makubwa yametokea ya jinsi mfumo mzima wa anuani za tovuti mbalimbali zinasimamiwa. Kwa kiasi flani tunaweza sema serikali ya Marekani imepoteza umiliki wa intaneti.

ICANN

Nini kimetokea?

Jumamosi hii serikali ya Marekani kupitia Wizara yake ya Biashara imeipa rasmi shirika la ICANN mfumo wa mzima wa usimamiaji wa teknolojia ya intaneti.

“Shirika la kimataifa la ICANN linahusisha usimamiaji kutoka wawakilishi wa kiserikali takribani 111 kutoka mataifa mbalimbali duniani.”

ICANN ni nini na hali ilikuwaje hapo mwanzo?

Kwa miaka mingi tokea ujio wa intaneti mfumo mzima wa anuani za tovuti mbalimbali umekuwa ukiendeshwa na kusimamiwa na shirika lisilo la kiserikali lifahamikalo kama IANA la nchini Marekani.

IANA ni mamlaka iliyokuwa inasimamia undikishaji wote wa anuani za kimitandao – yaani ‘domain names’.. hawa ndio wanaohakikisha pale unapoandika www.teknokona.com kwenye kompyuta ua simu yako ni tovuti ya Teknokona ifunguke na si tovuti nyingine.

Tayari shirika la ICANN lilikuwa linalojumuhisha wawakilishi kutoka mashirika makubwa na pia serikali mbalimbali kama vile China, Urusi n.k zilikuwa zinahusishwa katika usimamiaji wa mfumo mzima wa intaneti kupitia IANA kwa kipindi cha takribani miaka 20.

ICANN iliundwa takribani miaka 20 iliyopita ikiwa ni lengo kufikia miaka michache baadae ichukue usimamiaji wa mfumo wa IANA nje ya usimamizi wa Marekani. Lakini bado Marekani wakawa wagumu kidogo kutekeleza jambo hili.

Uvujaji wa siri kuhusu kiwango kikubwa cha udukuzi na ujasusi unaofanywa na mashirika la Usalama na Kijasasi ya Marekani (NSA na CIA) uliovujishwa na Edward Snowden uliharakisha zaidi madai kutoka mataifa mengine ya kutaka ICANN ichukue usimamizi wa teknolojia hiyo muhimu kwa mataifa mengi zaidi.

Kuna mapingamizi mengi yalifanyika nchini Marekani hasa hasa kutoka wanasiasa wa chama cha Republican hii ikiwa ni pamoja na ata kufungua kesi mahakamani za kuzuiana kukamilishwa kwa umiliki wa mfumo wa IANA kwa ICANN lakini zimeshindwa.

Makao makuu ya shirika la ICANN bado yapo Marekani na hivyo wanaopinga wameambiwa wasihofu kwani uwepo wa makao makuu ya shirika hilo Marekani linamaanisha haliwezi kuvunja sheria za kimataifa hasa hasa zinazoweza husisha kulazimishwa kitu na mataifa kama China na Urusi.

Vyanzo: Mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Fikiria Simu Bila Ya Betri, Teknolojia Hii Ipo Katika Hatua Zake Za Kwanza!
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com