Infinix na toleo la Infinix Note 4 Pro

2
Sambaza

Katika moja ya makapuni ambayo simu zake zinaonekana kupata soko zuri sehemu nyingi duniani Infinix ni moja ya makampuni hayo tofauti na zile kampuni ambazo tumezoea kuzisikia kwa kuleta ushindani wa vuta ni kuvute kwenye biashara.

Infinix imeshatoa matoleo mengi tu ya simu janja mpaka hivi leo lakini leo katika makala hii tunaiangazia uzuri wa simu janja ya Infinix Note 4 Pro ambayo imepata mwitikio mzuri wa kununuliwa na watu wengi tu ndani na nje ya Uchina. Simu kutoka Infinix zimekuwa zikiiweka kampuni hiyo katika ushindani wa kibiashara pamoja na makampuni mengine.

Sifa kuu za Infinix Note 4 Pro.

>Uwezo wa kuchaji haraka. Katika simu janja ya Infinix Note 4 Pro ina teknolojia ya kuiwezesha simu kujaa chaji haraka ndani ya muda mfupi. Ikiwa na teknolojia ya XCharge 4.0 inayoweza kuchaji simu hii kwa dakika 5 na mtumiaji akaweza kuongea kwa zaidi ya dakika 250 bila simu kuisha chaji.

>Diski uhifadhi/RAM. RAM ambayo ni kuingo muhimu sana kwenye simu/kompyuta kuifanya ichukue muda mchache kuweza kumaliza ile kazi iliyoamriwa na kama simu ina RAM ndogo basi itakuwa inachukua muda kuweza kumaliza kazi moja. Infinix Note 4 Pro ina RAM GB 3 na kiwango hiki cha RAM kimeboreshwa tofauti na matoleo ya nyuma ya Note Pro.

Kwenye diski uhifadhi ni moja ya sifa kuu katika simu ya Infinix Note 4 Pro na hapa simu hii imeboreshwa vilivyo kwa kuwekwa GB 32 za ujazo wa ndani na kuweza kukubali uhifadhi wa ziada wa mpaka GB 128.

>XPen (Kalamu ya kijanja). Hali imekuwa ni tofauti tangu simu ya Infinix Note 4 Pro iwe nayo na kalamu ya kijanja kwenye simu hiyo inayofahamika kama XPen ambayo inaweza kufanya chaguzi za aina yake (smart select), kutumika kuandikia kwenye memo, sms, n.k.

Infinix Note 4 Pro imeondoa kile ambacho kilikuwa kimezoeleka machoni pa wengi kwa kuona simu za “Note” ndio tu zilikuwa na kalamu.

Sifa nyinginezo za Infinix Note 4 Pro.

 >Ukubwa na ubora wa kioo. Katika simu janja nyingi siku hizi zinakuwa na kioo chenye ukubwa wa kuridhisha ili kumpa uwanja mpana mtumiaji kuweza kufurahia simu yake ya mguso hata kama akiwa na vidole vinene. Kioo cha kwenye Infinix Note 4 Pro kina ukubwa wa inchi 5.7 na ubora wa kioo ukiwa 1080 x 1920 pixels.

>Prosesa/Programu endeshaji. Infinix Note 4 Pro inatumia prosesa ya Octa inayoifanya simu hiyo kuwa nyepesi wakati wa kuperuzi mtandaoni au hata wakati wa kucheza gemu na kuifanya simu kutokuwa nzito. Simu hii inatumia XOS 2.2 pamoja na Android Nougat 7.0.

>Uwezo wa betri/Bei yake, Katika simu janja ni muhimu sana betri yake iwe na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu ili kuepuka kuishiwa nachaji baada ya saa chache tu baada ya kujaa na chaji. Betri la kwenye Infinix Note 4 Pro ni la Li-ion lisilotoka lenye nguvu 4500mAh. Bei yake ni zaidi ya Tsh. 420,000.

SOMA PIA:  Samsung J7 Inaweza Kuwa Ya 1 Kuja Na Kamera Mbili Za Nyuma Kutoka Samsung!

Sifa

Uwezo

 Kamera Kamera ina MP 13 pamoja na flash 2, kamera ya nyuma ina MP 8
Aina ya kioo IPS LCD
Usalama Ina teknolojia ya fingerprint iliyowekwa eneo la mbele
Laini za simu Inakubali laini 2
Wembamba 159.6 x 78.8 x 8.3mm (uzito ni gramu 200)
Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni Ina ukubwa wa 3.5mm
Rangi Kahawia, nyeusi, dhahabu na bluu
Mnara/Teknolojia nyinginezo GPRS, Edge, 3G HSPA, 4G LTE, Bluetooth v4.0, Wi-Fi 802.11 b/g/n, hotspot, Micro USB na ina redio
SOMA PIA:  Fanya Simu Yako Ya Android Au iOS Itaje Jina La Mpigaji, Ukipigiwa!

Infinix Note 4 Pro ni simu yenye uwezo wa juu tu na kwa hakika imevutia zaidi kwa kuwa na kalamu spesheli kama zilivyo simu za Samsung kutoka familia ya Note. Wewe je, una maini gani kuhusu simu hii?

Vyanzo: Techweez, What Mobile, Naija Android Arena

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com