Ondoa tatizo la ‘An Unknown Network Error Has Occurred’ katika Instagram

0
Sambaza

Instagram ni moja ya programu maarufu zaidi duniani katika mitandao ya kijamii. Programu hii imetoa njia nzuri ya watu, ndugu na marafiki kuwasiliana na kufahamishana kupitia picha na ujumbe kiasi.

Lakini wakati mwingine programu hii imekuwa ikiwasumbua wengi kwa kuleta hitilafu inayowafanya wasiweze kutumia Instagramu kama kawaida.

Moja ya hitilafu ambayo imekuwa ikijitokeza kwa wengi ni pale mtu anapojaribu kufungua hugoma na kumletea ujumbe huu, “An Unknown Network Error Has Occurred”

Kwa wale ambao wamepatwa na tatizo kama hilo leo tutakufahamisha namna ya kuondoa.

1. Izime na uiwashe simu yako

SOMA PIA:  Twitter yaleta kipengele kipya kwenye mtandao wake

Njia ya kwanza zima simu yako na uiwashe tena.Wakati mwingine kuzima simu na kuwasha tena
huweza kutatua tatizo hilo na mengine. Ikiwaka jaribu kuingia Instagram

2. Angalia Intaneti.

Mara nyingine tatizo hilo hujitokeza pale panapokuwa na hitilafu ya Inataneti yako
kutokuwa sawa au ikiwa katika kasi ndogo sana. Jaribu kuweka sawa intaneti yako na ujaribu
kufungua tena.

3. Futa cache katika programu ya Instagram.

Kufuta cache na data

Wakati mwingine Cache katika program inaweza kuwa imeharibiwa hivyo kuonesha hitilafu. Basi jaribu kufuta cache katika Programu.

SOMA PIA:  Sasa unaweza kuagiza chakula Facebook.

Namna ya kufuta ingia Settings Kisha Application(Apps) utaona App nyingi tafuta Instagram ifungue na ubonyeze palipoandikwa Clear Cache na Clear data. Baada ya kumaliza bonyeza Force Stop. Kisha zima simu yako na uiwashe tena.

4. Angalia tarehe na muda (Date and Time)

unknown network error

katika simu yako. Baadhi ya matatizo katika simu kutokana na tarehe na muda kutokuwa sawa. Kuweka sawa ingia Settings halafu Date & Time. Ukishaingia rekebisha vizuri tarehe na saa. kisha weka Automatic Date and Time.

5. Fanya Update ya Instagram.

Namna ya kufanya Update

wakati mwingi makosa katika programu hurekebishwa kwa kufanyiwa maboresho na masahihisho (Update). Cha kufanya ingia katika Play store na uandike Instagram itafunga page na upande wa kulia utaona pameandikwa Update. Utabonyeza hapo na itanedelea mpaka itamaliza itakupa fursa ya kufungua Instagram ikiwa haina tatizo hilo. Ikiwa hakuna update basi ifute (Unistall) kisha uipakue uipakuwe upya

SOMA PIA:  Google Assistant sasa inaweza kujua jina la wimbo unaoimba kwenye simu janja #Masasisho

Hizo ndio baadhi ya mbinu au njia za kurekebisha tatizo hilo katika Instagram linalosema “An Unknown Network Error Has Occurred”.

Tunatarajia umepata ufumbuzi wa tatizo lako. Hebu tujuze ni njia gani iliyofanya kazi kwako. Tupe maoni yako hapo chini.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com