Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu

1
Sambaza

Jambo la kuweka neno siri/nywila imekuwa ni kitu ambacho kimezoeleka na pengine mtumiaji hatojihisi yuko salama kama hatoweka nywila kwenye simu yake.

Udukuzi unaweza ukafanyika hata bila ya wewe kutarajia kama mtu angeweza kufahamu password yako ila tambua ya kwamba jinsi unavyoshika simu janja yako kunaweza kumfanya mtu mwingine akajua neno siri unalotumia kwenye simu yako kwa urahisi.

Katika utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Newcastle ulibaini kuwa asilimia 70 ya nambari zote za siri zenye tarakimu nne zilifahamika baada ya kujaribu mara moja tu na kwa asilimia 100 baada ya kujaribu mara tano.

Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu

Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu: Hakuna kampuni ya teknolojia iliyopata suluhu ya tatizo la programu zinazoiba data muhimu.

Simu nyingi aina ya simu janja na tabiti zimewekwa sensa ingawa kuna tovuti nyingi na programu za simu haziombi ruhusa kabla ya kutumia programu hizi jambo linalopelekea kuwa rahisi sana kwa programu mbaya kupata taarifa kutoka kwenye simu husika.

SOMA PIA:  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

Wataalamu wamegundua kwamba kila unachofanya katika simu iwe ni kupiga simu, kuandika ujumbe mfupi wa maneno au kutafuta kitu hupelekea mtu kuishika simu kwa njia fulani ya kipekee.

Ni muhimu kwa mtu kuhakikisha anatengeneza nywila ambayo si rahisi mtu kubahatisha kuifahamu au hata akijaribu kukutazama wakati unapoiweka basi iwe ngumu kwake kuweza kuikariri.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com