Utafiti: Bei ya Simu Janja yaendelea kupanda zaidi mwaka hadi mwaka

0
Sambaza

Kama ulisikia taarifa ya bei inayotarajiwa kuuzwa simu mpya ya iPhone X iliyotangazwa mwanzoni mwa mwezi huu bila shaka ungerudi nyuma kidogo!

Simu hiyo kutoka kampuni ya Apple inatarajiwa kuuzwa zaidi ya dola 999 za kimarekani kuanzia Novemba 3 mwaka huu, na kuifanya kuwa moja wapo ya Simu Janja ghali zaidi duniani. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa mwenendo wa kuendelea kupanda kwa gharama za bei ya Simu Janja umekuwa ukikua mwaka baada ya mwaka.

Kulingana na utafiti ulitolewa na kampuni utafiti kwa walaji ya kijerumani ya Gesellschaft für Konsumforschung (GfK) kwa wastani wa mauzo ya Simu Janja yanakuwa kote ulimwenguni.

Utafiti: Bei ya Simu Janja yaendelea kupanda zaidi mwaka hadi mwaka

Taarifa inasema kumekuwa na ongezeko kwa asilimia 7 katika robo ya tatu ya 2017, ikilinganishwa na robo ya tatu ya mwaka 2016. Takwimu hizo zinatofautiana sana kutoka soko moja kwenda lingine.

Soko la Marekani linaongezeko kwa asilimia 1 kwa wastani wa upandaji wa bei tofauti na soko la Ulaya ya kati na Mashariki ambapo inaonesha kuna ongezeko kwa asilimia 26 ya upandaji wa bei ya Simu Janja. Kumbuka soko kwa Amerika ya kaskazini nalo ni kubwa, hawa wanaongezeko la asilimia 1.

Hata hivyo, takwimu zinaonesha kwamba watumiaji wa Simu Janja ghali wameongezeka kuliko ilivyokua awali kwa ulimwenguni kote. Soko la mashariki ya kati na Afrika kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya simu kwa asilimia 8 kila mwaka sambamba na ongezeko la bei ya Simu Janja kukua kwa asilimia 5.

SOMA PIA:  Mwanamuziki 50 Cent atengeneza mabilioni kupitia fedha za kidigitali! #BitCoin

Takwimu hizi zimeegemea zaidi ya masoko 75 yaliyofanyiwa utafiti huo kati ya mwezi Agosti na Septemba na bei zilizoangaliwa ni zile za kuuza na sio zile za wauzaji wa mwisho. Takwimu hizo zimeonesha kwamba bei ya simu janja zinaendelea kupanda mwaka hadi mwaka.

Pamoja na kuendelea kupanda kwa bei ya Simu Janja lakini uzalishaji wa baadhi ya simu kutoka China umekuwa una nafuu kwa kiasi fulani kwa watu walio wengi. Kupanda kwa simu kumeelezwa pia ni kwa baadhi ya watumiaji kuona fahari kutumia simu za bei ya juu ili kuonesha unadhifu na kujali kilicho bora.

SOMA PIA:  Kampuni ya Uber yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya

Kwa Tanzania mwenye kuhitaji simu Janja nzuri analazimika kununua kuanzia laki tatu na kuendelea kitu ambacho kwa mtu mwenye kipato cha chini hiyo ni bajeti inayoumiza. Hata hivyo, bei hizo kwa soko la Tanzania limeendelea nalo kuwa na ongezeko kubwa kutokana na athari ya soko la Ulaya na Marekani.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com