FutureBrand mara nyingi huwa inafanya utafiti ili kujua ni kampuni gani bora zaidi duniani. Mara nyingi huwa makampuni yanaangaliwa kwa mtazamo wa haraka haraka ni si kwa mali ilizonazo.
Hii inatoka na kwamba mara nyingi utafiti huo unafanyika na maswali ambayo yataliwezesha kampuni kujipatia nafasi kati ya zile 100 bora huwa yanaulizwa kwa wateja.
Kwa mwaka huu (2016) kampuni ya Apple imejipatia nafasi ya kwanza kabisa. Tafiti inaonyesha mawazo ya watu kwa kampuni 100 za muhimu kwa kuangaza katika vipengele 18.
FutureBrand iliwahoji wateja juu ya mtazamo wao kuhusiana na makampuni makubwa duniani, wateja 3000 waliaulizwa watoe nafasi za makampuni hayo kulingana na vipengele walivyovitoa kama vile utu, bei, ubunifu na uaminifu.
Kampuni ya Apple imekuwa namba moja mwaka huu lakini kupitia kwa mawazo au maoni ya wanajamii. Pengine kama kila kitu kingeangaliwa na wataalamu isingeshika namba hiyo kwani duniani kuna makampuni makubwa kushinda Apple.
Kampuni ya pili katika utafiti huu ni lile la Bil Gates yaani Microsoft. Tafiti hizi zinasema japokuwa Apple imeipita Microsoft lakini bado kampuni hiyo ya Microsoft inaishinda Apple kwa ubunifu.
Baadhi ya makampuni mengine yaliyopata nafasi za juu ni Amazon, Disney, Samsung, Facebook na Toyota.