Utafiti: Watumiaji wa iPhone huwa ‘hawawapendi’ kimapenzi watumiaji wa Android

0
Sambaza

Upo hapo? Utafiti uliofanywa na tovuti ya Match.com nchini Marekani unaonesha watu utumia hadi vigezo vya simu ambayo mtu anatumia katika kuchagua mpenzi.

Inaonekana watumiaji wa iPhone ndio ‘wanaojisikia’ zaidi…na hivyo kuchukulia umiliki na utumiaji wa iPhone kama ni kiwango flani cha ubora wa mtu.

Utafiti huo uliusisha maswali yaliyojibiwa na takribani watu 5,500 ambao wapo ‘single’ na kwenye umri wa miaka 18 na zaidi.

Matokeo;

  • Watumiaji wa simu za iPhones wanaonekana ndio wanaangalia sana suala la simu ya mtumiaji pale wanapotafuta mpenzi, watumiaji wa Android huwa hawapendelewi zaidi.
  • Watumiaji wa iPhone wanauwekezakano wa zaidi mara 21 zaidi kuwa na mtazamo hasi kwa mtu kwa sababu anatumia simu ya Android kuliko pale wakikutana na mtu ambayo naye anatumia simu za iPhones.
  • Je unatumia simu iliyotoka miaka 10 iliyopita? Habari mbaya ni kwamba mtu anayetumia simu ya iPhone au ya android iliyotoka miaka mingi zaidi iliyopita ana nafasi ya zaidi ya asilimia 56 ya kukosa mpenzi pale atakapokutana na mtu anayetumia simu ya kisasa zaidi.
SOMA PIA:  Simu ya LG G6: LG waonesha bado wapo makini na biashara ya simu

Unapenda kulalamika lalamika Facebook?

  • Pia utafiti huo umeonesha asilimia 58 ya watu walioshiriki kwenye utafiti huo moja kwa moja hawapendi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wanaolalamika sana Facebook.
  • Pia asilimia 50 hawataki kuwa na mtu ambaye anatumia muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii.

Je kwa mtazamo wako, unakubaliana na vingapi kati ya hivi vilivyopatikana kwenye utafiti huu? Je unakubaliana na matokeo haya..

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: DigitalTrends.com

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com