Baada ya Kutumia Mabilioni, Jeshi la Marekani Lasita Utumiaji wa Roboti katika Ubebaji wa Mizigo

0
Sambaza

Jeshi la Marekani linaonesha kusita kutumia teknolojia ya maroboti spesheli katika ubebaji wa mizigo ya kijeshi baada ya kutumia mabilioni ya pesa katika utengenezaji wa teknolojia hiyo.

Kampuni ya Boston Dynamics (inayomilikiwa na kampuni ya Alphabet – kampuni mama ya Google) kwa miaka kadhaa imekuwa ikitengeneza na kuboresha maroboti spesheli watakaoweza kutumiwa na jeshi la Marekani kwa ajili ya kubeba mizigo mizito na kupitika sehemu ambazo magari ingekuwa shida kupita.

Roboti huyu anauwezo wa kubeba hadi KG 181 na kutembea umbali wa zaidi ya KM 30 bila kuitaji mafuta.

Roboti huyu anauwezo wa kubeba hadi KG 181 na kutembea umbali wa zaidi ya KM 30 bila kuitaji nyongeza ya gesi.

Teknolojia hii inayofahamika kwa jina la The LS3, yaani ‘Legged Squad Support System’ imekuwa ikifanyiwa kazi tokea mwaka 2008, jeshi la Marekani lilimewekeza zaidi ya dola milioni 30 za Kimarekani (Tsh bilioni 65+ au Ksh bilioni 3+) awamu ya kwanza, na baadae mwaka 2013 wakawekeza dola milioni 10. Kampuni ya Boston Dynamics imefanikiwa kutengeneza na kufanya maboresho kadhaa ya maroboti tokea mwaka 2008.

Uwekezaji huu wa pesa za walipa kodi katika teknolojia hii umetokea chini ya mpango mkubwa wa jeshi la Marekani la kuhakikisha hadi inapofikia mwaka 2030 kuwe na utumiaji wa maelfu wa maroboti katika majeshi yake.

Lakini ata baada ya utumiaji wa pesa zote hizi kitengo cha jeshi la Marekani cha Defense Advanced Research Projects Agency (DARPA) kinachosimamia utekelezaji wa programu hii kimesema teknolojia hii hadi sasa inakasoro moja tuu kubwa – KELELE! Katika utembeaji wa roboti hao kuna sauti inayotoka na sauti hiyo kwa wanajeshi waliofanya majaribio na maroboti hayo wanasema ni ya juu na inaweza sababisha adui kujua walipo kwa haraka.

Kelele zinahusishwa na utumiaji wa gesi kuendesha mitambo ya roboti huyo, njia rahisi ya kuondoa kelele ingekuwa kutumia betri za kuchaji ila tatizo ni kwamba utumiaji wa betri badala ya gesi utapunguza uwezo wa roboti huyo kubeba mizigo na kutembea kwa takribani mara 10 chini zaidi ukilinganisha na utumiaji wa gesi.

Roboti wa sasa ni wa toleo la tatu na tokeo toleo la kwanza hadi sasa sauti imepungua kwa kiasi kikubwa sana na kampuni ya Boston Dynamics inaamini wakiendelea kupewa muda basi maboresho makubwa zaidi yatafikiwa. Ila tayari kuna watu wengi wanaoona ya kwamba programu hiyo inakula pesa nyingi sana huku matokeo yakiwa madogo na yanayochukua miaka mingi.

Utumiaji wa roboti. Kupitia sensa spesheli roboti huyu ataweza kutembea akimfuata mtu mwenye kifaa spesheli kinachowasiliana naye. Roboti ataweza kutembea akikwepa vizuizi n.k

Kupitia sensa spesheli roboti huyu ataweza kutembea akimfuata mtu mwenye kifaa spesheli kinachowasiliana naye. Roboti ataweza kutembea akikwepa vizuizi n.k

Vyanzo kadhaa vinaonesha kuna uwezekano mkubwa wa programu hiyo kutoendelezwa kipesa tena na jeshi la Marekani, na hili likitokea basi litakuwa ni jambo baya kwa kampuni ya Boston Dyanamics ambayo kwa muda mrefu jeshi la Marekani limekuwa ni chanzo kikubwa cha pesa.

SOMA PIA:  FAHAMU: Mega Pixel (MP) Ni Nini Na Inafanya Nini Katika Picha!

Angalia video hii fupi inayoonesha jinsi gani roboti hao spesheli wanatembea.

Kampuni ya Boston Dynamics ilinunuliwa na Google mwishoni wa mwaka 2013, na sasa ipo chini ya ALPHABET

Je una maoni gani juu ya teknolojia hizi za kutumika kijeshi? Kumbuka lengo lao ni kwamba ifikapo mwaka 2030 wawe na maroboti wa aina mbalimbali wanaotumika jeshini…kwa kifupi teknolojia inazidi kutumika na kutegemewa kurahisisha mambo hadi kwenye sekta ya jeshi.

Vyanzo: Military.com, BetaBoston.com na vinginevyo.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com