Miezi kadhaa iliyopita tulishawahi kuandaaa makala kuhusu orodha ya nchi ambazo zinajishughulisha na uwekezaji/kufanya miamala kwa njia ya pesa zisizoshikika au kwa lugha rahisi sarafu za kidijitali, Tanzania nayo ipo kwenye orodha hiyo.
Kama moja ya teknolojia ambayo inakuwa kwa kasi nchi mbalimbali duniani zinatambua na kukubali mfumo wa malipo kwa kutumia sarafu hizo za kidijiti huku nyingine zikiwa kwenye mchakato wa kuzikubali. Kwa Tanzania pia watu kadha wa kadha wamewekeza huko kutokana na kuamini mfumo huo.
Jitihada zinazofanyika Tanzania kuleta mbele sarafu za kidijiti.
Kwa kuanza tuu ipo jumuiya (Blockchain Tanzania) ambayo inalenga kuelimisha umma/Watanzania kuhusu teknolojia iliyopo nyuma ya sarafu husika kwa maana ya kwamba mtu anaweza akawekeza na kupata faida baada ya muda fulani ila kabla ya kujiingiza huko basi ni vyema ukapata elimu na kuelewa kisha ufanye maamuzi ya kuwekeza.
Lakini bado yapo makampuni nchini Tanzania yanafanya biashara hiyo hata kuwa na sarafu zake zenyewe mathalani TemboCoin ambayo tayari inafanya kazi lakini pia iRA na sarafu yake ya Diligence ingawa bado haijaingia sokoni.
Kubwa zaidi hivi karibuni Belfrics Tanzania Limited walipata fursa ya kueleza mbele ya baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kuhusu faida sarafu za kidijitali na wengine serikali ikaweza kutambua kama njia mojawapo rasmi inayoweza kutumia kufanya miamala.
One Comment
Comments are closed.