Uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ya kubadili laini: Vitu muhimu vya kufahamu

0
Sambaza

Nadhani hadi sasa utakuwa umekwishapata taarifa ya uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ata ya kubadili laini/namba ya simu kama ilivyokuwa kwa muda mrefu kabla. Na tunaamini maswali yatakuwa mengi tayari.

Tanzania mitandao ya simu

Fahamu hapa mambo muhimu ya kujua;

Utaratibu wa kuhama mtandao huku ukibakia na namba ya simu ileile

Itakubidi ufike kwenye mtandao wa simu yako na ujazo fomu ya kuomba uhamisho, hatua ya pili itakuhusisha kuandika neno HAMA kwenye huduma ya SMS na kutuma kwenye namba 15080. Na utapata majibu kuhusu zoezi lako la kuhama mtandao.

SOMA PIA:  Firefox Send: Mozilla waja na huduma ya kutuma mafaili kwa usiri

Huwezi kuhama mtandao kama una deni kwenye mtandao unaouacha.

Hili limesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, hautaweza hamisha namba yako ya simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kama una deni la aina yeyote kwenye mtandao wa simu uliopo. Hii inamaanisha deni la vocha, au la huduma za pesa kama vile mkopo kwenye huduma ya TIMIZA Airtel na nyinginezo kama hizo.

Hakuna kuhama mtandao mara mbili ndani ya siku 30.

Ni lazima ukae kwenye mtandao uliopo kwa siku si chini ya 30 kabla ya kuomba tena kuhama mtandao wa simu.

SOMA PIA:  Bustani ya kidigitali yenye sauti mbalimbali za matunda yaundwa #Teknolojia

Wakati unahama…

Kipindi cha muda ambao namba yako inafanyiwa kazi kuhamishiwa mtandao mwingine huduma za kipesa za mtandao uliopo kama vile Airtel Money, MPesa, n.k zitasitishwa kwa muda huo na kurudishwa ukiwa tayari umehamia mtandao mpya. – ila huduma zingine zote kama vile kupiga na kupokea simu na sms zitafanya kazi kama kawaida.

Kwa kiasi tunategemea ujio wa teknolojia hii utaongeza ushindani kwa kiasi kikubwa sana.

Labda muda si mrefu mitandao yetu itatumia ofa za simu nzuri za kisasa za malipo madogo madogo kama sehemu ya kujihakikishia mtumiaji atakaa na mtandao wao kwa muda mrefu zaidi.

Vipi wewe unaongeleaje maendeleo haya?

SOMA PIA:  FastJet kupata ndege mpya, Embraer E190. Ifahamu Zaidi

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com