Uzinduzi wa Android O, hili ndio jina lake jipya!

0
Sambaza

Wakati kampuni ya Google jumatatu inatarajia kuzindua toleo jipya la Mfumo endeshi wa Simu janja wa Android tayari makisio ya wengi ya jina la toleo hilo yametolewa.

Toleo hilo kwa sasa linaitwa Android O kwa sababu jina litakuwa linaanzia na herufi O kwa mpangilio waliouweka wenyewe Google. Jina linalotarajiwa na wengi zaidi kupewa toleo hilo ni Oreo.

Wengi wameweka dhana hiyo baada ya kuvuja kwa faili la video lililoonekana na mtu aliyedai ameona jina la Oreo. Oreo ni aina ya Chokoleti tamu ambazo ni maarufu sana nchini Marekani

Chokoleti za Oreo

Hata hivyo inasemekana baada ya muda mfupi Faili hilo lilibadilishwa jina na kuwekwa Octopus (Pweza). Hata hivyo bado hakuna uhakika wa jina gani toleo hilo litabeba.

SOMA PIA:  Kivinjari cha UC Browser chaondolewa katika soko la Apps la Google PlayStore

Google imekuwa ikiyapa majina ya Pipi au Chokoleti matoleo yake ya Android kwa kufuatisha mpangilio sawia wa herufi.

Wengi hawataraji jina la toleo jipya kuwa Octopus kwani itakuwa ni kinyume na utaratibu wa utoaji wa majina ya matoleo ya Android, ambapo hutoa kwa kwa pipi na Chokoleti na si kwa vyakula vya baharini.

android o

Logo Ya Android O

Mbali na jina hilo la Oreo, majina mengine yanayotarajiwa pengine yanaweza kubeba jina toleo hilo la nane la Android ni Oatmeal, Orellete, Oatcake, OH Henry, Octopus, Olives, Omega spread, Oca, Ocean Perch, Oat milk nk.

SOMA PIA:  Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi

Toleo hilo jipya linatarajiwa kuwa na maboresho mengi mazuri ikiwemo ulaji mdogo wa chaji ya betri, Fonts mpya za kupakuwa na mengi mengi.

Endelea kutembelea Teknokona kwa kujua jina la toleo jipya la Android O na mengine mengi.

Msomaji wetu bado upo huru kukisia ni jina gani ambalo unahisi watalipa toleo lao la Android linalotarajiwa kutangazwa leo, jumatatu tarehe 21 Agosti mwaka huu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com