Vaio Waja Na Simu Janja Yenye Mfumo Wa Android!

0
Sambaza

vaiophone2-1024x683

Mwaka Mmoja umepita tangu Vaio (Visual Audio Intelligent Organizer) wapewe uhuru na kampuni ya Sony, Kampuni hiyo (vaio) ina mpango wa kuachia simu yake ya kwanza kabisa. Kabla ya vaio kununuliwa na ‘Japan Industrial Partners’  kampuni hiyo ilikua ikimilikiwa na kampuni mama yaani Sony.

Vaio kwa ujio wao wa kwanza kabisa katika simu, wamekuja na simu janja yenye Os ya Android. Bei ya simu hiyo imekadiriwa kuwa  kati ya dola za kimarekani 420.

v

Japokua simu hii ina tegemewa kuuzwa Japan tuu tena haswa kwa toleo hili. Ndani ya simu hii ya Vaio kuna prosesa ya ‘1.2 GHz quad-core ‘ ambayo inajumuisha ram ya GB2 na GB 16 za  memori kadi ya nje ambayo inaweza kuongezeka mpaka GB 64.

SOMA PIA:  Simu ndogo unayoweza 'Kuizungushazungusha'

Simu ina Kioo cha inchi 5 na kioo hicho ni cha  1280 x 720 HD (high definition), Kamera ya nyuma ina MP (Mega Pixels) 13, Na kamera yake ya Selfie (kamera ya mbele)  ina MP 5.

Simu hii ya Vaio ambayo itapatikana kwa rangi nyeusi ni nyembamba kwa kiwango cha 7.95 mm na ina ujazo wa gramu 130, betri yake ni ya 2,500 mAh.

Wateja wengi  bado wanazani Vaio wanaingiliana kwa namna flani na laptop za Sony. Vaio (Visual Audio Intelligent Organizer)  imeuzwa na Sony kwa kampuni nyingine ya Japan mwaka 2014 na hii ni baada ya kuuza biashara yake ya kompyuta kwa kampuni hiyo (Japan Industrial Partners).

SOMA PIA:  Ujenzi wa betri kubwa kuliko yote mpaka sasa wakamilika kwa 50%

b-vaio-a-20150313

Wakati wawekezaji wengi na  wachambuzi wengi wametoa mawazo yao kuwa sony wangeweza, wantakiwa waachane au wajitoe katika soko la simu ambalo linajumuisha simu janja na tablet, kampuni  hilo (sony) ndio kwanza limefumba masikio na hivi karibuni wametangaza bidhaa zao mpya.

Simu mpya ya Vaio inaonyesha hadharani kuwa kutakua na ushindani kati ya simu hiyo na zile za Sony za matoleo ya Xperia na watafanya hivyo katika uwanja wa nyumbani Japan. Inategemewa mafanikio ya toleo hili yanaweza kuwafanya kuingia katika soko la dunia kabisa.

SOMA PIA:  Google kutambulisha simu janja mbili mwezi Oktoba

VAIO-phone-710x481

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com