VETA kutoa elimu ustadi kwa njia ya simu! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

VETA kutoa elimu ustadi kwa njia ya simu!

0
Sambaza

Chuo cha elimu ya ufundi Stadi VETA kwa kushirikiana na mtandao wa Airtel kupitia mpango wake wa kijamii Airtel Fursa umezindua utaratibu wa kutoa elimu ustadi kwa vijana kwa kutumia simu. Njia hii inategemewa kufungua fursa kwa vijana wengi zaidi kuweza kujipatia mafunzo kwa njia ya mtandao.

http://themaatrust.org/?p=8

Huduma hii itapatikana kupitia app ambayo Airtel wameitengeneza na ambayo imepewa jina la VSOMO, baada ya kujiunga mtumiaji ataweza kusoma kozi mbalimbali na pindi atakapo kuwa amesoma asilimia 40 ya kozi yake (ambayo ni nadharia) mwanavunzi atatakiwa kujiandikisha katika chuo cha jirani cha VETA ili aweze kufanya masomo ya vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki mbili na baada ya hapo mwanafunzi atatakiwa kufanya mtiani ambao kama atafaulu basi atakuwa amefuzu kozi.

INAYOHUSIANA  Airtel Tanzania yajiunga mfumo wa malipo kwa GePG

buy femara australia Ingawa app hiii ya VSOMO ni bure na lakini mwanafunzi atatakiwa kulipia ada ya 120,000/= kwa Airtel money kwaajiri ya gharama za ada.

Mkuu wa chuo cha VETA kipawa akizungumza katika uzinduzi huo amesema kwamba ili kuhakikisha ubora wa wahitimu wanaotoka katika mpango huu wanafunzi wote watafanya mtihani baada ya kozi hiyo na ni wale to ambao watafaulu ndio watakao zawadiwa vyeti vya kuhitimu.

Kwa upande wa mwakilishi wa Airtel amesema kwamba njia ya masomo kwa mtandao ni rahisi na App ya VSOMO itapatikana kwa wateja wote wa Airtel ambao wanatumia Android ( wale wa iOS pengine itabidi wasubiri kidogo) na pia akasisitiza kwamba asilimia arobaini ya mafunzo haya ambayo itakuwa ni nadharia itakuwa bure lakini kumalizia elimu hii kwa vitendo itabidi mwanafunzi alipe ada yenye punguzo ambayo ni shilingi 120,000/=

VETA

Mkuu wa Airtel akizungumza katika ufunguzi huo

Hii ni nafasi kwa vijana wengi zaidi ambao kwa namna moja ama nyingine hawakuweza kupata elimu na wangependa kujipatia elimu ya ufundi stadi

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.