Vevo Imedukuliwa Taarifa Zenye Ukubwa Wa TB 3.12! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Vevo Imedukuliwa Taarifa Zenye Ukubwa Wa TB 3.12!

0
Sambaza

Kundi la wadukuzi maarufu linalojulikana kama OurMine ndio linalohusika na shambulizi hili la udukuzi wa mafaili katika mtandao wa Vevo.

buy cipro online overnight

Lamictal fedex Vevo  wamedai kuwa taarifa zenye ukubwa wa TB 3.12 ndio zimedukuliwa. Taarifa hizo zinahusisha Vedeo za miziki mbalimbali, nyaraka na taarifa zingine binafsi.

enter site Ujuzo huo wa data ni mkubwa sana na kama umefanikiwa kupatikana kwa mikono ambayo sio salama basi inabidi mtandao wa Vevo ufanye juu chini ili kuhakikisha ulinzi na usalama ni wa hali ya juu sana katika mtandao wako.

Mafaili Ya Vevo

Kuna mafaili katika taarifa hizo yalikua yemetengwa na kuandikwa “Premieres” ambayo kwa haraka haraka yanamaanisha kuwa ni mafaili ya utambulisho wa kitu (mfano Video mpya). Mbali na hapo taarifa nyingi za maswala ya masoko na zenyewe zilidukuliwa.

Vevo kwa upande wao walikiri kuwa udukuzi umetokea na wana fanya juu chini ili kuchunguza kwa lengo la kujua kuwa udukuzi huo ni mkubwa kiasi gani na pia kuweza kulizui  jambo kama hilo tena.

Katika upande wa OurMine wenyewe wamesema kuwa karibia kila mwezi huwa wanachagua makampuni fulani fulani hivi na kuweza kupima uzuri wa ulinzi wao (katika mtandao). Hivyo Vevo ilikua ni moja kati ya makampuni hayo.

Baada Ya Ombi Kutoka Kwa Vevo, OurMine Walifuta Taarifa Hizo Katika Mtandao Wao

Baada ya muda Vevo waliomba OurMine kuzitoa taarifa zao katika mitandao yao na OurMine walifanya hivyo. OurMine pia ni kampuni ambayo inatoa huduma za ulinzi na usalama katika mtandao kwa makampuni ambayo yanahitaji

OurMIne wao wamejitetea kuwa walipoweza kudukua taarifa walijaribu wasiliana na Vevo lakini Vevo waliwajibu vibaya na kusema kuwa hakuna chochote walichodukua, ndipo hapo wakaamua kupakia mafaili katika mtandao wao (OurMine).

OurMine wenyewe wanasema hakuna kampuni yeyote iliyosalama kwa wadukuaji, hata wao wenyewe hawako salama siku yeyote wanaweza wakadukuliwa.

Ningependa kusikia kutoka kwako, funzo hili wewe unalionaje? je ni vyema kuweka taarifa za watu waliodukuliwa katika mitandao ya wadukuaji? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwa Habari Za Kiteknolojia, Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.