Viber Wajiboresha, Waja Na Mfumo Mpya Wa Mawasiliano Wa Akaunti Za Biashara!

0
Sambaza

Viber ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambapo hapo awali ulikua na ushindani wa hali ya juu na mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Kwa sasa Viber imeonyesha dhahiri kuwa inataka kuweka urahisi wa watu wenye biashara zao kuongea na makampuni kwa urahisi kabisa bila ya kutumia namba zao za simu kama mwanzo.


Na jambo hili sio kwa Viber tuu bali kuna makampuni mengi yameonekana kwa kiasi kikubwa yakijitahidi kuboresha mawasiliano katika App zao yasiwe ni kupiga, kupokea simu na kutuma meseji tuu.

SOMA PIA:  YouTube GO - App ya YouTube isiyokula data sana

Ili mitandao kama hii ifanikiwe basi haina budi kujikuza zaidi, kumbuka mitandao hii sio kwa ndugu, jamaa na marafiki tuu – dunia imebadilika – hivyo hata wafanya biashara wanaitegemea kwa kiasi kikubwa sana. Na pengine jambo hili labda ndio limeifanya kampuni kuja na kipengele hiki.


Kwa kifupi ni kwamba mtandao wa Viber umetoa njia ya rahisi kabisa ya kuwasiliana na biashara Fulani kwa urahisi kabisa bila hata ya kupoteza muda kutafuta namba za simu za kampuni hilo.

SOMA PIA:  Roboti atakayeweza kushiriki tendo la kujamiiana! #Teknolojia

Ukitaka kutafuta na kuona habari za makampuni maarufu ya biashara utakuwa huna budi kuingia katika kipengele cha ‘Public’ na kisha uanze kujionea mwenyewe
Mazungumzo yako yote ya akaunti za biashara yatatokea eneo lile lile ambalo hata mazungumzo ya kawaida yanatokea.

Kingine kikubwa zaidi ni kwamba unaweza ukali’Follow’ kampuni Fulani kwa ajili ya kupata taarifa za haraka moja kwa moja kutoka katika kampuni hilo na mara nyingine unaweza hata ukapata ofa mbalimbali.

SOMA PIA:  Mkurugenzi wa Apple ameanza kutumia iPhone 8 ambayo haijazinduliwa rasmi?


Kumbuka karibia kila mtandao wa kijamii kwa sasa unaboresha au umeboresha namna watu wanavyoweza kuwasiliana katika mtandao huo. Viber wametoa toleo jipya katika iOs na Android ambalo ndio lina hiki kipengele.

Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushaanza kutumia huduma hii? Je unaichukuliaje niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka kutembelea TeknoKona kila siku kwa habari moto moto na maujanja mbalimbali kuhusiana na teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com