Viettel 'Halotel' Umeingia Kwenye Gemu, Je Utaweza Kupata Mafanikio - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Viettel ‘Halotel’ Umeingia Kwenye Gemu, Je Utaweza Kupata Mafanikio

0
Sambaza

Mtandao wa simu wa Halotel umezindua huduma zake hivi karibuni na umeingia ukiwa na lengo kuu la kuwa moja ya mitandao mikubwa kabisa nchini pale idadi ya wateja na mapato vikitumiwa.

Je uwezo huo wanao?

Tayari wanafungua maduka katika maeneo mbalimbali nchi nzima

Tayari unaweza kupata huduma zao nchi nzima

Uwezo wa kukua kwa kasi na ata kushika nafasi ya pili au na moja wanao, kwani wamefanikiwa kusambaza huduma zao kwa ukubwa zaidi kuliko mtandao mwingine wowote nchini. Wanadai wanawafikia asilimia 81 ya wananchi wote nchini na watu wengi hasa vijijini wamefikiwa na huduma ya simu kwa mara ya kwanza kabisa.

Kampuni mama inatambulika kwa jina Viettel na wengi walitegemea watumie jina hilo, lakini wakaamua wajiite jina jingine.

Pia sababu nyingine kubwa inayoweza wasaidia ni uamuzi wao wa kuweka mitambo ya kiwango cha 3G katika minara yao yote nchini. Kumbuka mitambo ya mitandao mingi ya sasa ina teknolojia ya 2G tuu katika maeneo mengine hasa hasa katika miji midogo na vijijini. Halotel watawapatia huduma ya 3G hadi vijijini.

Halotel umekuwa mtandao wa kwanza nchini kuwa na teknolojia ya kasi ya intaneti ya 3G nchi nzima

Halotel umekuwa mtandao wa kwanza nchini kuwa na teknolojia ya kasi ya intaneti ya 3G nchi nzima

Wameshajifunza kuanza wa mwisho na kukua kwa kasi katika kipindi kifupi – hii ni sababu nyingine kubwa inayoweza wasaidia kuwaletea mafanikio Tanzania. Viettel wamiliki wa mtandao wa Halotel washaanzisha huduma zingine za mawasiliano ya simu katika nchi mbalimbali Afrika hii ikiwa ni pamoja na Msumbuji na kuweza kukua kwa kasi na ata kushikilia namba moja katika baadhi ya nchi hizo.

INAYOHUSIANA  TCRA kuzifutia leseni DSTV na ZUKU

Soma zaidi – Fahamu kwa Nini Mtandao Mpya wa Simu wa Viettel Unaogopeka!

Je umefurahishwa na ujio wa kampuni hii ya simu? Tuambie unachotegemea kutoka kwao, na kama tayari ushanunua laini ebu tuambie unaonaje huduma zao hadi sasa.

Tulishawahi kuuliza na wengi walisema watajiunga na mtandao huo mara moja

[socialpoll id=”2280053″]

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply