Vodacom Kuuza Simu na Vinginevyo Kwa Bei Rahisi Jumamosi Hii - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Vodacom Kuuza Simu na Vinginevyo Kwa Bei Rahisi Jumamosi Hii

0
Sambaza

Mtandao wa simu wa Vodacom umeandaa tukio jingine la mauzo makubwa ya simu, tableti na vitu vingine vya elektroniki hapo kesho (Jumamosi).

“Njoo ujipatie simu kali kali kwa bei ya punguzo la hadi asilimia 75%. Hii siyo ya kukosa! Mwambie mwengine amwambie na mwengine na wote tukutane Jumamosi na Jumapili hii. KIINGILIO….BURE BURE KABISA au tuseme ni uwezo wako wa kufika.”

Kupitia Vodacom EXPO huwa wanauza vitu vingi kwa bei nafuu zaidi ukilinganisha na bei za kawaida na wengi huwa wanachukulia hatua hii kama moja ya jinsi ya wao kuanza upya, yaani kutoa kila walichonacho kabla ya kuagiza vifaa (simu, tableti n.k) mpya kila baada ya muda flani.

INAYOHUSIANA  Halopesa-Halopesa ni bure! Halotel-Mitandao mingine inavutia

Kwenye ukurasa wao wa Facebook wa tukio hilo la Vodacom EXPO, wamesema “Njoo ujipatie simu kali kali kwa bei ya punguzo la hadi asilimia 75%. Hii siyo ya kukosa! Mwambie mwengine amwambie na mwengine na wote tukutane Jumamosi na Jumapili hii. KIINGILIO….BURE BURE KABISA au tuseme ni uwezo wako wa kufika.”

Bonanza hilo la mauzo litafanyika katika viwanja vya posta Kijitonyama.

Bonanza hilo la mauzo litafanyika katika viwanja vya posta Kijitonyama.

http://yourultimatespeech.com/category/ultimate-speech/ Timu yetu ya TeknoKona itaenda maeneo hayo na tutakuambia baadhi ya simu kali zaidi tutakazoziona. Kama upo jijini Dar es Salaam na ulikuwa unafikiria kununua simu hivi karibuni tunakushauri utembelee pia, kwani unaweza kujikuta ukapata simu nzuri kwa bei nzuri sana.

INAYOHUSIANA  NMB, Halotel kutoa huduma za TEHAMA bure mashuleni

Chanzo | https://www.facebook.com/events/455535367947604/

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply