Waathiriwa wa Samsung Galaxy Note 7 wabadilishiwa simu

1
Sambaza

Samsung Galaxy Note 7 ni simu janja ambayo ni toleo jipya katika muendeleo wa familia ya Samsung galaxy Note. Imekuwa faraja kwa wateja waliokuwa wamenunua Samsung galaxy Note 7 ambazo zilipatikana kuwa na dosari baada ya muda fulani.

Simu ya Samsung Galaxy Note 7 iliodaiwa kuwa na betri zinazolipuka imeanza kubadilishwa Uingereza, soma zaidi.

Kampuni ya Samsung inataka wamiliki wa simu hizo walioathirika kuwajulisha waliowauzia, lakini wengi wa wafanyibiashara wa simu hizo wanasema tayari wanawasialiana na wateja wao moja kwa moja.

Simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 ilyolipuka.

Simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 ilyolipuka.

Wito umetolewa kwa wateja kupeleka simu hizo ili ziweze kubadilishwa haraka iwezekanavyo ambapo  Samsung galaxy Note 7 zenye betri ya kijani zilikuwa salama kutumia.

SOMA PIA:  Google AutoDraw: Sasa hivi mtu yeyote anaweza kuwa mchoraji mzuri

Hata hivyo ni wateja wachache tu ndio wameweza kukubaliwa kubadilishiwa simu zao kutokana na baadhi ya wateja hao (waliokataliwa kubalishiwa simu zao) kununua simu hizo sehemu nyingine au walinunua kupitia mtandaoni (online).

galaxy-note-7

Samsung galaxy note 7

Tangu simu hizo kupata matatizo mauzo yake yameshuka kwa 0.1% kuanzia mwezi Agosti kitu ambacho maka sasa kimesababisha hasara ya mabilioni ya dola duniani kote.

Ili mteja aweza kubadilishiwa simu yake anapaswa kuirudisha kwa mtu muuzaji halisi aliyemuuzia simu hiyo. Wateja ambao walikwisha ‘activate‘ simu zao wamepewa kipaombele.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com